Na Nova Kambota,
Niliwahi kutabiri huko nyuma kuwa siku Lowassa atakapofungua mdomo wake na kuzungumza basi hali ya kisiasa ya nchi itabadilika ghafla naam! Lowassa jana sio tu amezungumza bali amezungumzia sehemu sahihi ambayo ndiyo haswa alipopaswa kuyasema aliyoyasema, nani kasema kuwa kuna baadhi ya watu hawajavutiwa na hatua hii ya lowassa? bilashaka kitendo cha lowassa kusimama upande wa wananchi kwa kuponda utendaji mbovu wa serikali huku akipandikiza moyo wa kujiamini kama taifa kwaa mfano kutumia pesa tulizonazo kutatua matatizo yetu huku akikazia kwaa kibwagaizo cha ….“tujenge reli ya kati, tupanue bandari Tanga, DSM, pesa tunazo, tumejenga UDOM kwa pesa zetu wenyewe” hali iliyofanya baadhi ya wabunge kumpigia makofi, hapa kuna siri kubwa ambayo inaturudisha kwenye swali lisilojibiwa la TATIZO NI LOWASSA AU URAIS 2015?
sasa mimi nasema hivi Kikwete lete utamu sasa mambo yazidi kunoga! ila hii ni vita na hainaa macho lazima mmoja ashinde na mawingine ashindwe hivyo mwisho wa yote haya kuna mmoja atajeruhiwa tu kisiasa lakini ndiyo hivyo tena hakuna jinsi hii ni safari ya kuwaweka huru wote wawili JK na Lowassa kwani sasa kwa mbali naona wameanza sfari ndefu ya kuutafuta UKWELI.
Na
Novatus Kambota
No comments:
Post a Comment