Balozi wa Ireland nchini Loccam Fullam(katikati) akiwasili katika Banda la Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) kwa ajili ya kuangalia na kujifunza shughuli mbalimbali zinazoendeshwa na shirika hilo katika kuwaletea wananchi maendeleo.
Balozi wa Ireland nchini Loccam Fullam(kulia) akikaribishwa na Meneja Mawasiliano wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Neema Mbuja (kushoto) jana jijini Dar es salaam wakati alipotembelea banda la Shirika hilo kwenye maonyesho ya 35 ya kimataifa ya biashara ya Dar es salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerereili kujionea shughuli mbalimbali wanazozifanya.
Balozi wa Ireland nchini Loccam Fullam(katikati) akipata maelezo mafupi kuhusu mradi wa uzalishaji wa chuma ghafi eneo la Maganga Matiti , Ludewa mkoani Njombe jijini Dar es salaam kutoka kwa Meneja wa Mradi huo Abdallah Mandwanga(kulia) wakati Balozi huyo alipotembelea Banda la Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) kwenye maonyesho ya 35 ya kimataifa ya biashara ya Dar es salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere. Kushoto ni Meneja Mawasiliano Neema Mbuja. Mradi huo unasimamiwa na Maganga Matitu Resources Development Limited.
Balozi wa Ireland nchini Loccam Fullam(katikati) akipata maelezo mafupi kutoka kwa Mtaalamu wa Miamba(Geologist) wa Kampuni ya TANCOAL Alex Sosteness(kulia) kuhusu mradi wa machimbo ya makaa ya mawe wa Mbalawala wilayani Mbinga unaotarajiwa kuanza uchimbaji hivi karibuni.Mtaalamu huyo alitoa maelezo hayo wakati Balozi huyo alipotembelea NDC kwenye maonyesho ya 35 ya kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam. Kushoto ni Meneja Mawasiliano wa Shirika la Maendeleo la Taifa Neema Mbuja.Picha na Tiganya Vincent
No comments:
Post a Comment