KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Thursday, 30 June 2011

ZITTO KABWE AWASILISHA USHAHIDI WAKE KWA SPIKA

Friday, 1/07/2011

WAKATI Ofisi ya Bunge ikigoma kumsaidia Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kupata nyaraka za Kikao cha Baraza la Mawaziri kwa ajili ya kuthibitisha madai yake kuwa Baraza hilo limerubuniwa, mbunge huyo amewasilisha kurasa nne za ushahidi huo akitumia dokezo la kikao hicho cha siri.

Habari zilizopatina na kuthibitishwa na Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel zilisema kuwa Zitto aliwasilisha ushahidi huo kwenye Ofisi ya Bunge jana mchana, huku taarifa zaidi zikionyesha kuwa aliwasilisha ushahidi huo ukiwa na hoja tatu kuthibitisha madai yake.

Kwa mujibu wa habari hizo, mbunge huyo aliwasilisha ushahidi wake uliosomeka “Tofauti kati ya mapendekezo ya Waraka wa Barazaa la Mawaziri na Pendekezo la Azimio la Bunge lililoletwa bungeni kuhusu kuongeza muda wa Shirika Hodhi la Mali za Mashnirika ya Umma, yaani Consolidated Holding Corporation (CHC)" .

"Amewasilisha ushahidi wake leo, uko hapa unafanyiwa kazi," alisema Joel alipoulizwa na gazeti hili.

Juzi, Spika Anne Makinda alimwongezea muda Zitto hadi Jumatatu Juni 4 mwaka huu, kuthibitisha madai yake hayo baada ya kueleza kuwa alishindwa kufanya hivyo juzi, Juni 29 kutokana na ofisi ya Spika kugoma kumsaidia kupata nyaraka za Kikao cha Baraza la Mawaziri kwa kuwa ni siri.

Akithibitisha hoja zake katika ushahidi huo ambao gazeti hili umefanikiwa kuuona, Zitto alisema, Azimio la Bunge lililowasilishwa bungeni na Serikali kabla ya marekebisho lilitaka CHC iongezewe muda wa mpito wa miaka mitatu na baadaye kazi zitakazokuwa zimebaki zipelekwe kwenye Ofisi ya Msajili wa Hazina ni tofauti na mapendekezo ya kitaalamu yaliyofikishwa mbele ya Baraza la Mawaziri.

Kwa mujibu wa maelezo ya Zitto, waraka wa wataalamu ulikuwa na mapendekezo ya aina mbili na kwamba hakuna hata pendekezo moja katika mapendekezo hayo lililozungumzia CHC kuongezewa muda wa miaka mitatu.

"Pendekezo la kwanza linalopatikana katika Aya ya 11.0 ya waraka huo, lilitaka CHC ifanywe kuwa taasisi ya kudumu. Pendekezo la pili linalopatikana katika Aya ya 12.0 ya waraka huo, liligusia mpango mbadala wa kuiongezea CHC muda wa miaka 5," ilisema sehemu ya ushahidi huo.

Katika ushahidi huo, Zitto alisema Aya ya sita ya Azimio la Bunge ilianza kujenga hoja ya kutaka CHC iongezewe muda wa mpito na baadaye majukumu yake yahamishiwe kwenye Ofisi ya Msajili wa Hazina. Alisema aya hiyo ilisomeka hivi:

"Na kwa kuwa Serikali inatambua umuhimu wa kuiongeza muda wa mpito wa shirika na Serikali inaandaa na kukamilisha utaratibu wa kuhamishia majukumu ya CHC kwenye Ofisi ya Hazina.

"Wakati Azimio lililoletwa bungeni lilijenga hoja hiyo ya kutaka majukumu ya CHC yaje kuhamishiwa kwenye ofisi ya Msajili wa Hazina, Waraka wa Baraza la Mawaziri katika pendekezo lake la pili, umetahadharisha kuwa mpango wa kuhamishia kazi za CHC kwenye ofisi ya Msajili wa Hazina, utakabiliwa na changamoto kubwa,"ilisema sehemu ya ushahidi huo.

Ushahidi wake huo kwenye hoja ya tatu ulisema kuwa, wakati Azimio hilo lililoletwa bungeni (kabla ya kurekebishwa) lilijikita katika kutaka CHC iongezewe miaka mitatu na baadaye majukumu yake yahamishiwe kwenye ofisi ya Msajili wa Hazina, hitimisho la waraka uliowasilishwa kwa Baraza la Mawaziri katika Aya ya 13 linasomeka:

"Waheshimiwa mawaziri, mnombwa kutafakari mapendekezo yaliyomo kwenye Aya ya 11 ya waraka huu na kumshauri Mheshimiwa Rais ayakubali na aagize utekelezaji wake

"Hivi ni dhahiri kuwa Baraza lamawaziri lilikiuka maoni na ushauri wa wadau na watalaamu wote waliotaka CHC ifanywe kuwa taasisi ya kudumu; na dhahiri kuwa Seriakli ilikiuka mapendekezo na sababu zake zote za msingi zilizowasilishwa katika kikao hicho ambazo zilitaka CHC ifanywe kuwa taasisi ya kudumu" inahitimisha taarifa hiyo.

Juni 23 mwaka huu wakati anachangia Azimio hilo, Zitto alisisitiza mara tatu kwamba Baraza la Mawaziri limerubuniwa kufikia hatua hiyo na akawataka wabunge kwa umoja wao kutokubali kupitisha azimio hilo kwa kuwa lipo kwa maslahi ya watu.

"Waheshimiwa wabunge, nawaombeni kwa umoja wetu tulikatae azimio hilo, hicho sicho tulichokubaliana kufanya. Tayari tumeiagiza CHC kufuatilia madeni yetu kwenye kampuni za umma halafu leo, tunataka kuliua shirika hili? alihoji Zitto kabla Spika Makinda hajamtaka athibitishe kauli hiyo.

Kadhalika, wakati Makinda akimwongezea Zitto muda wa kuthibitisha madai yake alisema “Waheshimiwa wabunge itakumbukwa kuwa tarehe 23 mwezi huu Mheshimiwa Zitto wakati akichangia Azimio la Serikali kutaka kuliongezea uhai Shirika Hodhi la Mashirika ya Umma (CHC), alitoa tuhuma bungeni kwamba Baraza la Mawaziri, limerubuniwa kufikia maamuzi hayo."

Aliongeza: "Itakumbwa pia kuwa baada ya kauli hiyo, nilimtaka (Zitto) alete ushahidi ifikapo tarehe 29 Juni yaani leo. Sasa kwa kuwa siku yenyewe ya kuleta ushahidi ni leo, naona bora nitoe taarifa rasmi kwenu."

"Kwamba siku ileile ya tarehe 23, Mheshimiwa Zitto aliniandikia barua kuniomba nimsaidie kumpatia nyaraka za Kikao cha Baraza la Mawaziri kilichopitisha uamuzi huo. Amefanya hivyo kwa kutumia Kanuni ya Haki, Sura na Madaraka ya Bunge zinazompa haki mbunge kuiomba ofisi ya umma kumpa nyaraka anazozihitaji.

Hata hivyo, Makinda alisema, ofisi yake haikuweza kumpatia Zitto nyaraka hizo kwa kuwa vikao vya Baraza la Mawaziri ni siri na nyaraka zake zote hazitolewi kwa umma.
.

ZITTO AFICHUA UFISADI MADINI

1st July 2011
Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe
Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, ameshauri Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kukagua mapato katika sekta ya madini ya miaka 10 iliyopita, kutokana na jumla ya mapato yaliyolipwa na makampuni ya madini kwa serikali kubainika yalikuwa na tofauti ya Sh. bilioni 20.
Zitto alisema kuwa kiasi ambacho wawekezaji walidai kuwa walilipa kama kodi kilikuwa pungufu ya Sh. bilioni 20 kulinganisha na kiasi kilichoelezwa na serikali.
Alitoa ushauri huo wakati akichangia mjadala wa bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha wa 2011/2012, bungeni, mjini hapa jana.
Alisema tofauti hiyo ilitokana na ripoti iliyotolewa na Taasisi iitwayo Extractive Industries Transparency Initiative (EITI) baada ya kukagua malipo yaliyofanywa na makampuni ya madini kwa serikali mwaka huo.
Zitto alisema ushauri huo ni muhimu kutekelezwa kwani utasaidia kuepuka ugonjwa unaoikumba nchi ya Nigeria, ambako fedha zinalipwa kama mapato ya serikali, lakini zinaishia kuingia mifukoni mwa watu binafsi.
Alisema mamlaka husika ya serikali ilipoulizwa na Kamati ya

Kudumu ya Bunge ya Mashirika ya Umma (POAC, ambayo yeye (Zitto) ni mwenyekiti wake, ilidai kuwa nyaraka zinazohusiana na suala hilo zimechomwa moto.
Alisema baada ya ushuru wa mafuta ya taa kuongezwa kutoka Sh. 52 hadi 400.30, serikali inapaswa sasa kutoa agizo ushuru huo upelekwe kwa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ili ukasaidia umeme vijijini.
Alisema wakati wa bajeti kulikuwa na malalamiko mengi yaliyotolewa na baadhi ya wabunge kuhusu misamaha ya kodi, lakini serikali ilishikilia msimamo wake kwamba, lazima misamaha hiyo iendelee.
Hata hivyo, alisema kuna msamaha wa kodi uliotolewa na serikali, ambao anadhani serikali haikufikiria vizuri katika kuutoa.
Alisema jambo hilo alilijadili vizuri kwenye Kamati ya Fedha na Uchumi na kwamba, alitarajia kuwa lingebadilishwa kwenye Bunge lilipokaa kama kamati ya matumizi, lakini haikufanyika.
Alisema Waziri Mkuu alikutana na makampuni ya kutafuta mafuta nchini wakamuomba kwamba, waondolewe kodi katika mafuta wanayotumia katika kutafuta mafuta kwa madai kwamba, jambo hilo litasaidia uwekezaji zaidi.
Hata hivyo, alisema kwa sasa hivi kwenye eneo la utafutaji mafuta na gesi hakuna wa kushindana na Tanzania na pia serikali haiwezi kutoa vivutio kama ambavyo Kenya wanatoa, kwani wana makampuni manne yanayotafuta mafuta wakati Tanzania ina makampuni zaidi ya 22.
Alisema pia Tanzania haiwezi kutoa vivutio kama Msumbiji wanavyotoa, kwani faida pekee waliyonayo (Msumbiji) ni gesi waliyoigundua, ambayo iko kusini mwa Mkoa wa Mtwara. Zitto alisema kitu, ambacho serikali inatakiwa kukifanya ni kuhakikisha kiwanda cha gesi (LNG plant) kinajengwa haraka iwezekanavyo kabla Msumbiji hawajafanya hivyo.
Alisema Tanzania haitakuwa na faida ya kutoa vivutio kwa mafuta ya makampuni, ambayo yanatafuta madini, kwani itapoteza fedha bila sababu ya msingi.
"Na jambo hili ni la kuangalia kwa sababu kwenye mikataba yetu ya mafuta tuna vitu viwili; kuna kitu kinaitwa profit oil na coast oil. Coast oil maana yake ni kwamba kampuni ya mafuta ikishapata mafuta inatoa gharama zake zote, wanajilipa. Wakishajilipa zile gharama za mafuta yaliyoabaki ya ziada ndio tunayogawana,” alisema.
Mbunge wa Viti Maalum (Chadema-Morogoro), Suzan Kiwanga, aliitaka serikali kubadili utaratibu wa chai ofisi zake ili fedha zilizotengwa kwa ajili hiyo zipelekwe kugharamia miradi ya maendeleo.
Mbunge wa Viti Maalum (Chadema-Mbeya), Naomi Kaihula, aliitaka serikali kutumia rasilimali zilizopo kuanzisha mfuko wa kuwatunza watoto nchini.
Mbunge wa Viti Maalum (Chadema-Pemba), Raya Ibrahim Khamis, alisema anasikitishwa kuona Wazanzibari wakisahaulika kwenye kitabu cha hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

BALOZI WA IRELAND NCHINI ATEMBELEA BANDA LA SHIRIKA LA MAENDELEO YA TAIFA (NDC) VIWANJA VYA MAONYESHO YA BIASHARA SABASABA

Balozi wa Ireland nchini Loccam Fullam(katikati) akiwasili katika Banda la Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) kwa ajili ya kuangalia na kujifunza shughuli mbalimbali zinazoendeshwa na shirika hilo katika kuwaletea wananchi maendeleo.
Balozi wa Ireland nchini Loccam Fullam(kulia) akikaribishwa na Meneja Mawasiliano wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Neema Mbuja (kushoto) jana jijini Dar es salaam wakati alipotembelea banda la Shirika hilo  kwenye maonyesho ya 35 ya kimataifa ya biashara ya Dar es salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerereili kujionea shughuli mbalimbali wanazozifanya.
Balozi wa Ireland nchini Loccam Fullam(katikati) akipata maelezo mafupi kuhusu mradi wa uzalishaji wa chuma ghafi eneo la Maganga Matiti , Ludewa mkoani Njombe jijini Dar es salaam kutoka kwa Meneja wa Mradi huo Abdallah Mandwanga(kulia) wakati Balozi  huyo alipotembelea Banda la Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) kwenye maonyesho ya 35 ya kimataifa ya biashara ya Dar es salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere. Kushoto ni Meneja Mawasiliano Neema Mbuja. Mradi huo unasimamiwa na Maganga Matitu Resources Development Limited.
Balozi wa Ireland nchini Loccam Fullam(katikati) akipata maelezo mafupi kutoka kwa Mtaalamu wa Miamba(Geologist) wa Kampuni ya TANCOAL Alex Sosteness(kulia) kuhusu mradi wa machimbo ya makaa ya mawe wa Mbalawala wilayani Mbinga unaotarajiwa kuanza uchimbaji hivi karibuni.Mtaalamu huyo alitoa maelezo hayo wakati Balozi huyo alipotembelea NDC kwenye maonyesho ya 35 ya kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam. Kushoto ni Meneja Mawasiliano wa Shirika la Maendeleo la Taifa Neema Mbuja.Picha na Tiganya Vincent

Nape Nnauye Atembelea Vyombo Vya Habari Vya Mwananchi na Global Publishers

Nape akizungumza na wafanyakazi wa Global Publishers katika chumba cha habari cha Global. Wengine ni Mrisho, Ndauka, Sixtus na Ally.
Katibu wa NEC, Itikati na Uenezi, CCM, Nape Nnauye akizungumza na Wahariri wa magazeti ya Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, alipofaya ziara katika ofisi za kampuni hiyo, Tabata Dar es Salaam.Wa pili kulia ni Katibu Msaidizi Mkuu wa Idara ya Itikadi na Uenezi, Sixtus Mapunda na  Kshoto ni Mhariri Mtendaji wa kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, Theophil Makunga,Mhariri Mrendaji gazeti la Mwananchi Dennis Msacky, na Mhariri wa Mwanaspoti Frank Sanga.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM,Nape Nnauye(kulia) akikumbatiana kwa fraha na Mhariri Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Mwananchi, Daniel Msacky,alipotembelea ofisi za Mwananchi Communications Ltd, Tabata, Dar es Salaam, 29/6/2011. Kushoto ni Katibu Msaidizi Mkuu wa Itikadi na Uenezi CCM, Sixtus Mapunda.
                                       Mhariri wa Habari wa Mwananchi, yahya Charahani akiwa kazini.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akisalimiana na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Global Publishers, wachapishaji wa magazeti ya Uwazi, Kiu, Ijumaa na Champion, Abdallah Mrisho, baada ya kuwasili Ofisi za kampuni hiyo,Mwenge, Dar es Salaam.jana. Wapili kulia ni Mhariri Kiongozi wa kampuni hiyo    na Mhariri Kiongozi Oscar  Ndauka na Mwandishi wa kampuni hiyo Luqman Maloto na wapili kushoto ni Katibu Msaidizi Mkuu wa Idara ya Itikadi na Uenezi, Sixtus Mapunda.
Nape akiwa katika ofisi za Global Publishers.Kushoto ni  Abdallah Mrisho Wengine kutoka kulia ni, Sixtus Mapunda, Maloto,Ndauka na Mhariri kiongozi wa michezo wa Global Saleh Ally.Picha Zote na Mdau Bashir Nkromo

Waziri Mkuu Mizengo pinda na Mheshimiwa Luhaga Mpina wa Kisesa

Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Kisesa,Luhaga Mpina kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Juni 30,2011.Picha na Ofisi ya Waziri Mk

Mdau Nova Kambota Mwanaharakati Na Porojo Za Tatizo La Umeme Nchini

William Ngeleja waziri wa Nishati na Madini
---
 
Na Nova Kambota
 
Kama kuna jambo linalowaumiza vichwa watanznia basi ni swali kuwa kwanini kila wanalopanga halifanikiwi? au kwanini wananchi ni masikini licha ya maliasili zilizojaa kila kona yanchi hii? Wakiangalia elimu hoi watoto wanafeli, wakija kwenye afya hakuna kitu, wakienda kwenye kilimo na hata umeme tabu tu kwa kifupi hakuna jipya ni uduni na ubabaishaji mtupu.

 Katika lindi la mawazo ya namna hii au maswali mengi yasiyojibika tunawatazama viongozi wetu na uwajibikaji wao usiokidhi viwango kiasi kwamba wamepwaya mno , wajuzi wa kuzungumza bila kutenda, ni watu wa blah blah na porojo tu.

   Kwakweli Tanzania imetawaliwa na wapiga porojo hebu angalia kwenye hiyo kaulimbiu ya “kilimo kwanza”inavyotangazwa na kupigiwa chapuo na viongozi wetu kasha nenda huko vijijini kwenye mashamba utaona hata mabwana shamba hakuna na hizo pembejeo zenyewe za kilimo hakuna, sasa utasema hapo kuna kilimo kwanza au porojo tu?

    Geukia elimu nddio utashangaa kabisa kulivyooza huko lakini cha ajabu ni kuwa viongozi wetu bado wna ujasiri wa kusimama kwenye majukwaa na kudai kuwa serikali imeboresha elimu, elimu gani? Shule za kata? Si ndio hizi zinatoa sifuri? Nasikia siku hizi zinaitwa mtambo wa sifuri, ajabu sana! Yaani serikali inajenga majengo tupu bila walimu,madawati wala maabara kasha wanaita sekondari halafu wanazidi kuboronga wanafuta mitihani, tuziiteje hizi? Hizi ni porojo za watawala wetu, porojo porojo kila mtu anapiga porojo tu.
   Njoo kwenye hizo huduma za afya , tunaambiwa kuwa Tanzania bila maralia inawezekana tena kwa mbwembwe kwa matamasha makubwa lakini hivi mtu wa kule kijijini analala chini hana hata hiko kitanda je hiyo neti atachomeka wapi? Au motto wa mtaani analala kwenye vichochoro huyu neti atachomeka wapi? Sasa hizo Zahanati za vijijini kama kweli zinaviwango mbona vifo vya akina mama wajawazito bado vinaendelea? Hakika hizi ni porojo za viongozi wetu!

   Halafu anaibuka kiongozi mkubwa wa nchi anadai msongamano wa magari jijini Dar es salaam ni ushahidi wa kukua kwa uchumi wetu, hizi sasa porojo, uchumi wetu na nani? Mafisadi? Au Brigedia Al Adawy na Dowans? Uchumi umekua na ombaomba wameongozeka ndiyo magari yameongezeka na umasikini umekithiri , sasa huo uchumi uliokua umemnufaisha nani? Mawaziri na wabunge? Au rais na waziri mkuu? Hizi ni porojo tupu.
   Serikali nayo imeshindwa kuweka huduma za nishati ya umeme wa uhakika, sasa naona ina mchoko naam! Huu ni mchoko ndio maana kila kwenye hotuba tunapigwa kalenda mpaka mwaka huu au ule tatizo la umeme litakuwa historia halafu mda huohuo umeme ni wa mgao, waziri wa nishati nay eye hana jipya bado watu tunateseka kwa sababu ya kukosa ubunifu na uzalendo , mwenyekiti wa kamati ya bunge ya nishati anataka tuwashe mitambo ya Dowans, watu wanahoji anataka turudi tulipotoka? Hizi kama sio porojo nini basi? Nchi ipo gizani viongozi wanapiga porojo inasikitisha sana.

    Tabia ya kupiga porojo inaendelea kudidimiza nchi , hata kwenye michezo tunapiga porojo halafu tunataka kucheza kombe la Dunia,bungeni kuna porojo kiasi kwamba bunge linafanywa sehemu ya kupigana vijembe na mipasho halafu na sisi tunaamini iko siku tutakuwa kama wenzetu wa Ulaya na Marekani ambao tayari wamefuta blah blah na porojo kwenye kamusi za vichwa vyao wanafanya mambo kizalendo na kwa kujituma, haiwezekani !

    Matokeo ya porojo yanapoonekana viongozi wetu hawachelewi kusikitika na kuhidi kujirekebisha, ona matokeo ya kidato cha nne yalivyowaumbua viongozi sasa wanajifanya wamejifunza hakuna kitu porojo tu , mabasi yanakimbia yanavyotaka wenye jukumu la kulinda usalama barabarani wanapiga porojo watu wanakufa utadhani ni msimu wa ajali.

   Siku hizi hadi viongozi wa dini wamekumbwa na tabia ya kupiga porojo , badala ya kutetea wanyonge wao wanagombana wenyewe kwa wenyewe, wengine wanaenda mbali zaidi kwa kujigeuza miungu watu wanadanganya masikini na kuwakamua hata kidogo walichonacho na wengine wamejigeuza watabiri wanatabiria watu kufa? Hizi ni porojo tupu.

    Sasa katika muktadha huu ndio maana najiuliza kuwa nchi hii iliyolewa kwa wingi wa porojo itaendelea vipi?  Badala ya kwenda mbele sisi tunarudi nyuma kwasababu ya porojo zisizokwisha na hazina mipaka hata kwenye mambo ya msingi tunapiga porojo au ndio tunategemea  kuendelea kwa miujiza ya Mussa?  Tafakari!

Nova Kambota Mwanaharakati,
Tanzania, East Africa,
June 30, 2011

Waziri Mkuu Mizengo Pinda Akiteta Jambo na Joseph Simbakalia

Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akiteta na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma,Joseph Simbakalia kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Juni 29,2011.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu