Katika sherehe iliyofanyika Ikulu ya White House kumkaribisha kiongozi wa China Hu Jintao, amesema Marekani na China zitakuwa na ufanisi na usalama zaidi zitakaposhirikiana pamoja.
Bwana Obama pia alizungumzia suala tete la haki za binadamu.
Bwana Hu alisema ushirikiano huo unapaswa kuwa kwa misingi ya kuheshiminiana na pia kuheshimu mifumo ya maendeleo ya mwenziwe.
Viongozi hao wamekuwa wakijadili masuala yanayohusika na sarafu na biashara pamoja na ulinzi na usalama.
Maafisa wa Marekani wamefichua kwamba Marekani imetia saini mkataba wa dola za kimarekani billioni 45 kuiuzia bidhaa China , mkiwemo ndege 200 za muundo wa Boeing .
Mwandishi wa BBC mjini Washinton Paul Adams alisema serikali ya Marekani inahakikisha kwamba ziara hii inapewa kila makaribisho yanayostahili.
Baada ya kuwasili kwa Bwana Hu, viongozi hao walipeana mikono na kisha kiongozi wa China alikaribishwa kwa heshima kamili za kijeshi.
Wakati wa sherehe hizo upande wa pili wa White House waandamanaji wanaotetea uhuru wa Tibet walionyesha hamasa zao dhidi ya kile wanachokiona kuwa ni utawala wa ukandamizaji... Wakipiga makelele ---: "nani muongo? Hu Jintao ni muongo " na "muuaji ,muuaji, Hu Jintao."
No comments:
Post a Comment