Aliyewahi kuwa Rais wa Haiti, Jean Claude "Baby Doc" Duvalier, amesema kurejea kwake ghafla nchini humo baada ya kuishi uhamishoni kwa miaka 25, ni kwa sababu anataka kusaidia kuijenga upya nchi yake.
Katika taarifa yake kamili tangu arejee siku ya Jumapili, pia alionyesha masikitiko yake na huzuni kwa wale ambao wanajiona waliathirika enzi za utawala wake.
Matamsnhi yake yanajitokeza wakati kukiwa na msukosuko wa kisiasa nchini humo, ambao ulisababisha kufutiliwa mbali kwa awamu ya pili ya uchaguzi wa Rais.
Siku ya Ijumaa, Marekani iliwanyang'anya hati za kuingilia nchini mwake maafisa kadhaa wa Haiti, ikiwa ni sehemu ya kuichagiza serikali kumtupa nje ya kinyag'anyiro mgombea inayempendelea katika uchaguzi huo wa marudio.
No comments:
Post a Comment