WASEMA KAMA AMESHINDWA UWAZIRI AACHIE NGAZI
Mwandishi Wetu
WENYEVITI wa Kamati za Bunge za Nishati na Madini, January Makamba na Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), Zitto Kabwe wamesema ikiwa hali ya umeme itaendelea kuwa mbaya nchini, itamlazimu Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja kujiuzulu.Kadhalika, wenyeviti hao wamesema hakutakuwa na uhalali wa Serikali kuzilipa kampuni zilizopewa jukumu la kuzalisha umeme wa dharura ikiwa umeme huo hautapatikana katika muda uliotarajiwa.
Wakizungumza Dar es Salaam juzi usiku kwenye mdahalo kuhusu ‘Hali ya Umeme nchini na Tanzania tunayoitaka’ ulioandaliwa na Kampuni ya Vox Media, wabunge hao waliuponda mpango wa dharura wa Serikali wa kukabiliana na mgawo wa umeme wakisema hautekelezeki.Katika mdahalo huo uliorushwa moja kwa moja na Kituo cha Televisheni cha Star, January alisema: “Bora kutokuwa Waziri kuliko kuwa waziri ambaye kauli zake haziaminiki kwa umma.” soma zaidi,www.kwanzajamii.com
No comments:
Post a Comment