KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Thursday, 20 October 2011

Vodacom Tanzania Na Mkutano Wa Uongozi Na Namna ya Kufanya Kazi na Makundi Mbalimbali ya Watu

Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Stellah  Kiwango akitoa mada kuhusu Uongozi na namna ya kufanya kazi na makundi tofauti ya watu katika Mkutano wa siku moja ulioshirikisha wafanyakazi wa idara mbalimbali za Kampuni hiyo uliofanyika jijini Dar es salaam.
Mmoja wafanyakazi wa Vodacom Tanzania Bw. Charles Erasto akiuliza swali juu ya mada zilizojadiliwa katika  mkutano ulioshirikisha wafanyakazi wa idara mbalimbali za Kampuni hiyo wa uongozi na namna ya kufanya kazi na makundi tofauti ya watu.
Wafanyakazi wa Kampuni ya simu za mkoni ya Vodacom kutoka Idara mbalimbali wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa katika mkutano wa uongozi na nama ya kufanya kazi na makundi mbalimbali ya watu uliofanyika jana jijini dar es salaam.
Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Stellah  Kiwango (kushoto) akisalimiana na mmoja wa wafanyakazi wenzake ikiwa ni sehemu ya utambulisho wakati wa Mkutano wa siku moja wa Uongozi na namna ya kufanya kazi na makundi mbalimbali ya watu uliofanyika jijini  Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa masuala ya uongozi ambao pia ni wafanyakazi wa Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuhitimisha mkutano wao wa siku moja uliofanyika jijni Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment