Edward Lowasa
--
HOTUBA YA MBUNGE WA MONDULI,EDWARD LOWASA KWA WAANDISHI WA HABARI MONDULI, OKTOBA 19,2011.
NDUGU wana habari nimewaita katika mkutano huu leo kwa sababu moja kubwa, kutoa ufafanuzi kuhusu matukio ambayo yamekuwa yakitokea huku yakinihusisha mimi binafsi kwa namna ambayo sasa yanatishai ustawi na mshikamano wa kimaadili, kihistoria na kikazi miongoni mwa viongozi na baina ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi(CCM).
Ndugu wana habari, naamini mmekuwa mkifuatilia kwa karibu habari zinazoripotiwa katika baadhi ya vyombo vya habari zinazolihusisha jina langu na harakati kadha wa kadha chafu ambazo hata mimi mwenyewe ninayehusishwa nazo huwa nazisikia na kuzijua baadaya kuwa zimesharipotiwa katika vyombo vya habari.
Uamuzi wangu kukutana nanyi leo hauna makusudi ya kuzozana na vyombo vya habari wala kwenda kinyume na utamaduni wakimaadili wandani ya chama changu unaaotutaka viongozi kujadili masuala yanayokihusu chama chetu ndani ya vikao vyetu rasmi vya kimaamuzi bali kutoa ufafanuzi na angalizo kwa pande zote hizo ambazo zinaguswana matukio yanayoendelea kutoka leo hii.
Moja ya mambo ambayo yameligusa jina langu kwa namna hiyo ni lile linalonihusisha eti na kundi moja la wanasiasa ambao wamekuwa na mikakati ya kumhujumu mwenyekiti wetu wa chama, Mheshimiwa Rais Jakaya Kiwete. Hakuna shaka ni madai ya kipuuzi, kizishi na yenye malengo machafu.
Hawakuishia hapo sasa wamefikia hatua ya kuvitumia vyombo hivyo hivyo vya habari na kufikia hatua ya kudai kwamba nimeanza kuandaa orodha ya kile wanachokiita madhambi ya Rais Kikwete ambayo wanadai nimepanga kuyasoma wakati wa kikao kijacho cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (CCM).
Ninaamini kwa dhati kabisa kwamba, waandishi wa habari wanaofuatilia kwa karibu na kwa umakini mwenendo wa masuala ya kisiasa nchini wanatambua kwamba, watu wanaopenyeza taarifa hizi katika vyombo vya habari wanafanya hivyo kwa malengo ya kufikirika ya kujisafisha njia kisiasa.
Nijambo lisiloingia akilini kunihusisha na kile kinachoitwamikakati ya kumhujumu rais au chama ambacho mimi ni kada wake wa mudamrefu, mbunge anayetokana na chama hicho hicho na mtu ninayeiongoza Kamati nyeti ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama na zaidi ya yote kiongozi wa ngazi mbalimbali za kisiasa na kiserikali nilizowahi kushika.
Kuhusu hili napenda kusema kwa uwazi kwamba, mbali ya ukweli kuwa sijapata kufikiria hata mara moja kuhusu hicho wanachokiita mabaya au madhambi ya rais, sina na wala siijui hiyo wanayoiita kuwa ni orodha ya mabaya ya namna yoyote ya Rais Kikwete.
Mbali ya ukweli kwamba huo ni uongo wa wazi, silica yangu kama mwanasiasa na mtu mwenye dhamana kubwa kwawatu wa Monduli na kwa taifa langu haiwezi kamwe kunituma nianze kupanga mikakati ya kumhujumu kiongozi wetu mkuu au chama ambacho kimenilea na mimi mwenyewe nakitumikia kwa uadilifu na kwa juhudi kubwa pengine kuliko ilivyo kwa hao wazushi.
No comments:
Post a Comment