KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Wednesday, 19 October 2011

Daktari Mtanzania Julie Makani Atunukiwa Tuzo Kutoka Royal Society Pfizer London


                                                   Dr Julie Makani akitoa machache
Dr Julie Makani akiwa na Baba yake Mr Bob Makani pamoja na Mama Vicky Makani
                                                   Dr Julie Makani akiwa na familia yake.
Dr Julie Makani Akipokea Tuzo yake

Parliamentary Under Secretary of State, International Development Stephen O'Brien. akimpongeza Dr Julie Makani

                        Dr Julie Makani. akiwa na Cleo, Paul na Frank baada ya kupokea Tuzo

Kutoka Kulia Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Peter Kallaghe, Mama Makani, Dr  Makani, MP O'Brien, Naibu Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Chabaka na Mr Simba
                                Wageni waalikwa kwenye Royal Society Pfizer Awards London.

----
 Salaam,          

 Dr Julie Makani kutoka Tanzania amepokea Tuzo  jumanne tarehe 18 octoba 2011 ya Royal Society Pfizer nchini Uingereza. Dr  Makani amepokea tuzo hii ya utafiti alioufanya katika gonjwa hatari la Sickle Cell (SCD) ambaye makazi yake ya kazi ni kwenye Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi cha Muhimbili katika idara ya Haematology. Kutokana na utafiti wake kumeonekana ushahidi kuwa, chanzo kukuu cha magonjwa na vifo vitokanavyo na sickle Cell nchini Tanzania husababishwa na Arnemia (upungufu wa damu)
 Dr Makani pia amefanya mchakato wa matibabu katika majaribio ya Hydroxyure chemotherapy agent inayo gusa Bone marrow katika matibabu ya  Anaemia kwenye  ugonjwa Sickle Cell

Ni matumaini yake  kuwa utafiti huu utapelekea kuboresha uchunguzi na matibabu ya ugonjwa huu ili kuweza kuimarisha afya za watu, mfumo mzima wa afya  na jamii kwa ujumla.

Kwa niaba ya Watanzania  wote  Urban Pulse tunapenda kumpongeza  DR Makani kwa mafanikio hayo.

Asanteni 


Urban Pulse Creative

No comments:

Post a Comment