KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Sunday, 9 December 2012


RAIS DK. JAKAYA MRISHO KIKWETE AONGOZA WATANZANIA KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 51 YA UHURU WA TANZANIA UWANJA WA UHURU


Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dk.Jakaya Kikwete akiwasili katika gari maalum la Kijeshi na Mkuu wa majeshi Jenerali Davis Mwamunyange kwenye uwanja wa uhuru kwa ajili ya  maadhimisho ya miaka 51 Uhuru wa Tanzania Bara 2012 yanayofanyika kila mwaka Desemba 9, Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya Mwaka huu ni “Uwajibikaji, Uadilifu na Uzalendo ni nguzo ya Maendeleo ya Taifa letu”
(PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWEBLOG.COM)
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania Dk. Jakaya Kikwete akikagua gwaride la vikosi vya Ulinzi na usalaama katika maadhimisho hayo.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania Dk. Jakaya Kikwete akikagua gwaride la vikosi vya Ulinzi na usalaama katika maadhimisho hayo
Kikosi cha Brass Band cha majeshi ya Ulinzi na usalama  kikitumbuiza katika maadhimisho hayo
Viongozi mbalimbali wakiwa katika maadhimisha hayo kutoka kulia ni Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Mama Maria Nyerere, Rais wa Msumbiji Mh. Armando Guebuza,Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. Gharib Bilal na Mzee Ali Hassan Mwinyi rais Mstaafu wa awamu ya pili
Rais wa Msumbiji Mh. Armando Guebuza akipokewa  na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Said Meck Sadik mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Taifa.
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mh. Joseph Kabila akipokewa  na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Said Meck Sadik mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Uhuru asubuhi hii.
Mama Maria Nyerere akiwasili kwenye uwanja wa Uhuru kwa ajili ya kuhudhuria maadhimisho ya miaka 51 ya uhuru wa Tanzania.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Mizengo Pinda akiwasili kwenye uwanja wa Uhuru kuhudhuria maadhimisho hayo huku akisindikizwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Said Meck Sadik.
Mzee Ali Hassan Mwinyi akiwasili kwenye uwanja wa Uhuru kwa ajili ya kuhudhuria maadhimisho hayo.
Vikosi vya Ulinzi na Usalama vikiwa vimejipanga tayari kwa gwaride  la utii na heshima mbele ya Amiri jeshi Mkuu na Rais Jamhuri ya muungano ya Tanzania Dk. Jakaya Kikwete.
Makamu wa Rais Dk. Gharib Bilal akisalimiana na Mama Fatma Karume mara baada ya kuwasili uwanjani hapo, katikati ni Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda.
Rais Jakaya Kikwete akipokea gwaride la heshima wakati wa maadhimisho ya miaka 51 ya uhuru wa Tanzania Bara yanayofanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam akiwa pamoja na viongozi mbalimbali kutoka nje na ndani ya nchi
Rais Dk. Jakaya Kikwete kulia akipokea Gwaride la Heshima lililpokuwa likipita mbele yake wanaofuatia katika picha ni Rais wa Zanzibar Dk. Mohamed Shein, Rais wa Namibia Mh. Ifikepunye Pohamba na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakiwa katika maadhimisho hayo
Vijana wa chipukizi wakionyesha michezo na ujumbe mbalimbali wakati wa maadhimisho hayo.
Hapa wakionyesha ukakamavu wao huku wakiwa wameshika silaha.
Kikosi cha wanaanga Jeshi la wananchi JWTZ kikitoa heshima kwa gwaride kali mbele ya Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jakmhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. Jakaya Kikwete
Kikosi cha ardhini Jeshi la wananchi la Tanzania JWTZ kipita kwa gwaride la heshima mbele ya Rais Dk. Jakaya Kikwete.

Mkutano wa wakuu wa Nchi za SADC Jijini Dar 

Rais Jakaya mrisho kikwete, akikaribisha viongozi wenzie wa nchi za SADC katika  kikao cha dharura cha Jumuiya hiyo katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam  Desemba 8, 2012.
 Rais Jakaya mrisho kikwete, katika picha ya pamoja na  viongozi wenzie wa nchi za SADC katika  kikao cha dharura cha Jumuiya hiyo katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam  Desemba 8, 2012.
Rais Jakaya mrisho kikwete, Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini na  Rais Hifikepunye Pohamba wa Namibia pamoja na   Katibu Mkuu wa SADC Dr.Tomaz Salomao. na Mawaziri wa nchi hizo wakipitia rasimu ya muhtasari wa kikao kabla ya kuanza kwa kikao cha dharura cha Jumuiya hiyo katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam  Desemba 8, 2012. (Picha na IKULU).

Mh. Zitto ziarani Ulaya atakako hutubia Mkutano mkubwa wa masuala ya ushirikiano wa kiuchumi kati ya Ujerumani na Afrika.

Waziri Kivuli wa Fedha na Uchumi, Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mbunge wa Kigoma Kaskazini ndugu Zitto Zuberi Kabwe ameanza ziara ya kikazi nchini Ujerumani ambapo atahudhuria na kuhutubia Mkutano mkubwa wa masuala ya ushirikiano wa kiuchumi kati ya Ujerumani na Africa. Mkutano huo “Economic Conference: Commitment to Africa Initiative” utafanyika Jijini Berlin kuanzia tarehe 9 – 11 Desemba 2012 na umeandaliwa na Wizara ya Ushirikiano wa Kimaendeleo ya Serikali ya Ujerumani.
 
Katika ufunguzi wa Mkutano huo ndugu Zitto atatoa mada kuhusu mgongano wa maslahi kati ya Kampuni binafsi na Jamii ambapo ataongelea suala zima la makampuni makubwa ya kimataifa yanavyonyonya rasilimali za Afrika bila kuwajibika kulipa kodi na kuendeleza jamii zinazozunguka shughuli zao. Atazungumzia pia mitaji kiduchu inayokuja Afrika na fedha nyingi inayotoroshwa Afrika kupitia rushwa, ukwepaji kodi na wizi wa rasilimali. Afrika inapoteza zaidi ya dola za kimarekani 583 bilioni kila mwaka kutokana na utoroshaji wa fedha unaofanywa na makampuni ya kimataifa kwa kushirikiana na baadhi ya viongozi wa Afrika. Hata hivyo Afrika inapokea takribani dola za Kimarekani 80 bilioni tu kwa mwaka kutokana na Uwekezaji (FDI) na Misaada (foreign Aid). Tanzania ni moja ya nchi inayopokea misaada mingi kutoka nje na moja ya nchi ambayo rasilimali zake zinatoroshwa na baadhi ya viongozi wake kutorosha fedha na kuzihifadhi kwenye mabenki ya Ulaya kama Uswiss.
 
Mnamo tarehe 11 Desemba ndugu Zitto atakuwa kwenye jukwaa moja na Waziri wa Maendeleo wa Ujerumani kuzungumzia namna bora ya kushirikiana kati ya Ujerumani na nchi za Kiafrika. Miongoni mwa mapendekezo ya Zitto ni kuondokana na mfumo wa sasa wa ushirikiano wa misaada na badala yake kuwe na ushirikiano wa kujengeana uwezo ili kila nchi iweze kuhimili maendeleo yake yenyewe.
 
Katika ziara hii Zitto atakutana na Mawaziri Wakuu wa majimbo ya Nord Rhein Westphalen jimbo ambalo limefanikiwa sana katika vita dhidi ya ukwepaji kodi unaotokana na raia wa Ujerumani kuficha fedha kwenye mabenki ya Uswiss na wa jimbo la Lower Saxony kwa ajili ya mazungumzo kuhusu ukarabati wa Meli ya Liemba na kujenga mahusiano kati ya Mkoa huu na Mkoa wa Kigoma pia kati ya mji wa PapenBurg na Manispaa ya Kigoma.
 
Zitto anatarajiwa kutembelea baadhi ya nchi nyingine za Ulaya na kukutana na watu mbalimbali katika kuimarisha mtandao wa kimataifa dhidi ya utoroshaji wa fedha kutoka Afrika (illicit money transfer). Pia atakutana na watu binafsi wenye ujuzi na weledi katika masuala haya ya kupambana na watoroshaji wa fedha. Zitto anataraji kurudi nchini mnamo tarehe 16 Desemba 2012. Kwa namna itaakavyowezekana umma utapewa taarifa kuhusu ziara hii kupitia akaunti ya twitter na facebook ya ndugu Zitto. Pia mada zote atakazowasilisha zitawekwa kwenye blogu ya zittokabwe.com kila itakapowezekana.
 
Waziri Kivuli wa Fedha na Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni anawatakia Watanzania wote kila la kheri katika Sikukuu ya Uhuru wa Tanzania Bara. Utu, Uzalendo, Uadilifu na Uwajibikaji ni silaha muhimu sana za kujenga Taifa lenye heshima na jamii ya watu wenye fursa za kuendeleza maisha yao kwa haki na amani. Tutimize wajibu wetu katika kuijenga Tanzania tuitakayo kwa ajili yetu na kwa ajili ya vizazi vijavyo.
 
Imetolewa na Ofisi ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini.

Magazeti Leo Jumapili

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 


Kikundi Cha Akina Dada Wa Precious Group Chazinduliwa Rasmi

 

Mwenyekiti wa Kikundi cha akina dada cha Precious Group 2012 Agnes Shayo hiza akimkabidhi zawadi ya saa ya ukutani Magreth  Chacha ambaye ni Mkurugenzi wa benki ya wanawake (TWB)aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa kikundi hicho na chakula cha jioni iliyofanyika usiku huu kwenye ukumbi wa Isumba Lounge zamani Jolly Club jijini Dar es salaam, ambapo wageni mbalimbani na wanakikundi wa Precious walijumuika pamoja katika uzinduzi huo.
 
Mwenyekiti wa Kikundi cha akina dada cha Precious Group 2012 Agnes Shayo Hiza akimkabidhi tuzo maalum mgeni rasmi  Magreth  Chacha ambaye ni Mkurugenzi wa benki ya wanawake (TWB) katika hafla ya uzinduzi wa kikundi hicho uliofanyika kwenye ukumbi wa Isumba Lounge jijini Dar es salaam, kulia ni Jane Mchau mwanakikundi ambaye alikuwa ni MC katika hafla hiyo

   
Magreth  Chacha ambaye ni Mkurugenzi wa benki ya wanawake (TWB) akizindua rasmi kikundi cha Precious Groupkwenye ukumbi wa Isumba Lounge jijini Dar es salaam.
  
Magreth  Chacha ambaye ni Mkurugenzi wa benki ya wanawake (TWB) akifurahia jambo na  kikundi cha Precious Groupmara baada ya kukizindua rasmi usiku huu kwenye ukumbi wa Isumba Lounge.
  
Hapa ikabaki kuwa furaha kwa wote mara baada ya uzinduzi huo.
  
Magreth  Chacha ambaye ni Mkurugenzi wa benki ya wanawake (TWB) akiwapa nasaha wanakikundi wa Precious Group mara baada ya juzindua kikundi chao.
  
Mwenyekiti wa Kikundi cha akina dada cha Precious Group 2012 Agnes Shayo akizungumza na kukaribisha wageni katika hafla hiyo.
  
Christina Nyerere mshauri wa kikundi cha Precious Group akisoma risala mbele ya mgeni rasmi katika hafla hiyo.
  
Magreth  Chacha ambaye ni Mkurugenzi wa benki ya wanawake (TWB) akijadiliana jambo na Mweka hazina msaidizi wa kikundi hicho katika hafla hiyo, kulia ni Mwenyekiti wa Kikundi cha akina dada cha Precious Group 2012 Agnes Shayo

UN Yaendesha Semina Ya Mafunzo Juu Ya Haki Za Binadamu Kwa Wanahabari

 


Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania Hoyce Temu akitoa muhtsari kwa waandishi wa habari juu ya Taarifa kuhusu Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Msaada wa Maendeleo UNDAP 2011-2015 ambao unaelezea ushiriki wa Umoja wa Mataifa katika kuendeleza nyanja mbalimbali ikiwemo kupunguza umaskini wakati wa Semina ya kuwapa uelewa waandishi wa habari juu ya Haki za Binadamu tukielekea kwenye maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu Duniani itakayoadhimishwa tarehe 10 Disemba mwaka huu.

Mwezeshaji wa Semina hiyo Katibu wa Jukwaa la Wahariri nchini Neville Meena akitoa changamoto kwa wanahabari kutumia fursa mafunzo hayo katika kuhabarisha jamii kuhusu kazi zinazofanywa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini.

Mwakilishi Msaidizi wa UNICEF Bw. Paul Edwards akielezea nia ya Umoja wa Mataifa kuwakutanisha waandishi wa habari kila mwaka katika semina za mafunzo ambapo amesema jitihada za Umoja huo kutoa mchango katika juhudi endelevu za kupunguza umaskini na kupatikana kwa haki za Binadamu kulingana na visheni ya Maendeleo ya Taifa la Tanzania.

Mtalaam wa Program wa UNDP Bw. Amon Manyama akiwasilisha kwa wanahabari mpango kazi maalum wa miaka minne unaojulikana kama United Nations Development Assistance Plan 2011-2015 (UNDAP) uliotenga dola za Kimarekani Milioni 777 kwa Serikali ya Tanzania mpaka kukamilika ifikapo 2015.

Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa yasiyo na ukazi hapa nchini Bi. Aine Mushi akizungumzia jinsi mashirika hayo yanvyoweza kufanya kazi kwa pamoja ‘Delivering As One’ na Mashirika ya Umoja wa mataifa yenye ukazi hapa nchini.

Pichani Juu na Chini ni Washiriki wa Semina ya siku moja kutoka vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini.

Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mh. Mahfoudha Alley Hamid akizungumzia haki za msingi za Binadamu na wajibu wa vyombo vya habari katika kutetea haki hizo na kufichua pale zinapokiukwa ikiwemo kufuata maadili.
 
Afisa Mipango Mwandamizi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) Bw. Anthony Rutabanzibwa akitoa somo jinsi waandishi wa habari wanavyotakiwa kuripoti masuala yanayohusu hakiza Binadamu bila kutoka nje maadili ya kazi zao.
 
Pichani Juu na Chini ni baadhi ya washiriki wakichangia mada na kutoa maoni wakati wa semina hiyo.
 
 
Mwenyekiti wa timu ya Mawasiliano ya Umoja Mataifa Bw. Yusuph Al Amin wakati wa semina hiyo akifafanua jinsi sekta ya mawasiliano vikiwemo vyombo vya habari inavyoweza kuchangia maendeleo na kufanikisha kufuatwa kwa haki za binadamu.

Afisa habari wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi.Usia Ledama akitoa changamoto kwa wanahabari kusoma makabrasha yanayotolewa na mashirika mbalimbali ya umoja wa mataifa wakati wa mikutano na semina za kuelimishana kuhusiana na masuala mbalimbali yanayohusu jamii kwani kwa kufanya hivyo ndivyo watakavyoeweza kuelewa ushiriki wa Umoja wa Mataifa katika kupunguza umaskini na kutetea haki za binadamu.

Baadhi ya Maofisa wa Umoja wa Mataifa na Wanahabari wakati wa Semina hiyo.