RAIS DK. JAKAYA MRISHO KIKWETE AONGOZA WATANZANIA KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 51 YA UHURU WA TANZANIA UWANJA WA UHURU
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dk.Jakaya Kikwete akiwasili katika gari maalum la Kijeshi na Mkuu wa majeshi Jenerali Davis Mwamunyange kwenye uwanja wa uhuru kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 51 Uhuru wa Tanzania Bara 2012 yanayofanyika kila mwaka Desemba 9, Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya Mwaka huu ni “Uwajibikaji, Uadilifu na Uzalendo ni nguzo ya Maendeleo ya Taifa letu”
(PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWEBLOG.COM)
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania Dk. Jakaya Kikwete akikagua gwaride la vikosi vya Ulinzi na usalaama katika maadhimisho hayo.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania Dk. Jakaya Kikwete akikagua gwaride la vikosi vya Ulinzi na usalaama katika maadhimisho hayo
Viongozi mbalimbali wakiwa katika maadhimisha hayo kutoka kulia ni Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo , Mama Maria Nyerere, Rais wa Msumbiji Mh. Armando Guebuza,Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. Gharib Bilal na Mzee Ali Hassan Mwinyi rais Mstaafu wa awamu ya pili
Rais wa Msumbiji Mh. Armando Guebuza akipokewa na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Said Meck Sadik mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Taifa.
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mh. Joseph Kabila akipokewa na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Said Meck Sadik mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Uhuru asubuhi hii.
Mama Maria Nyerere akiwasili kwenye uwanja wa Uhuru kwa ajili ya kuhudhuria maadhimisho ya miaka 51 ya uhuru wa Tanzania.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Mizengo Pinda akiwasili kwenye uwanja wa Uhuru kuhudhuria maadhimisho hayo huku akisindikizwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Said Meck Sadik.
Vikosi vya Ulinzi na Usalama vikiwa vimejipanga tayari kwa gwaride la utii na heshima mbele ya Amiri jeshi Mkuu na Rais Jamhuri ya muungano ya Tanzania Dk. Jakaya Kikwete.
Makamu wa Rais Dk. Gharib Bilal akisalimiana na Mama Fatma Karume mara baada ya kuwasili uwanjani hapo, katikati ni Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda.
Rais Jakaya Kikwete akipokea gwaride la heshima wakati wa maadhimisho ya miaka 51 ya uhuru wa Tanzania Bara yanayofanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam akiwa pamoja na viongozi mbalimbali kutoka nje na ndani ya nchi
Rais Dk. Jakaya Kikwete kulia akipokea Gwaride la Heshima lililpokuwa likipita mbele yake wanaofuatia katika picha ni Rais wa Zanzibar Dk. Mohamed Shein, Rais wa Namibia Mh. Ifikepunye Pohamba na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakiwa katika maadhimisho hayo
No comments:
Post a Comment