UN Yaendesha Semina Ya Mafunzo Juu Ya Haki Za Binadamu Kwa Wanahabari
Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania Hoyce Temu akitoa muhtsari kwa waandishi wa habari juu ya Taarifa kuhusu Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Msaada wa Maendeleo UNDAP 2011-2015 ambao unaelezea ushiriki wa Umoja wa Mataifa katika kuendeleza nyanja mbalimbali ikiwemo kupunguza umaskini wakati wa Semina ya kuwapa uelewa waandishi wa habari juu ya Haki za Binadamu tukielekea kwenye maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu Duniani itakayoadhimishwa tarehe 10 Disemba mwaka huu.
Mwezeshaji wa Semina hiyo Katibu wa Jukwaa la Wahariri nchini Neville Meena akitoa changamoto kwa wanahabari kutumia fursa mafunzo hayo katika kuhabarisha jamii kuhusu kazi zinazofanywa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini.
Mwakilishi Msaidizi wa UNICEF Bw. Paul Edwards akielezea nia ya Umoja wa Mataifa kuwakutanisha waandishi wa habari kila mwaka katika semina za mafunzo ambapo amesema jitihada za Umoja huo kutoa mchango katika juhudi endelevu za kupunguza umaskini na kupatikana kwa haki za Binadamu kulingana na visheni ya Maendeleo ya Taifa la Tanzania.
Mtalaam wa Program wa UNDP Bw. Amon Manyama akiwasilisha kwa wanahabari mpango kazi maalum wa miaka minne unaojulikana kama United Nations Development Assistance Plan 2011-2015 (UNDAP) uliotenga dola za Kimarekani Milioni 777 kwa Serikali ya Tanzania mpaka kukamilika ifikapo 2015.
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa yasiyo na ukazi hapa nchini Bi. Aine Mushi akizungumzia jinsi mashirika hayo yanvyoweza kufanya kazi kwa pamoja ‘Delivering As One’ na Mashirika ya Umoja wa mataifa yenye ukazi hapa nchini.
Pichani Juu na Chini ni Washiriki wa Semina ya siku moja kutoka vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini.
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mh. Mahfoudha Alley Hamid akizungumzia haki za msingi za Binadamu na wajibu wa vyombo vya habari katika kutetea haki hizo na kufichua pale zinapokiukwa ikiwemo kufuata maadili.
Afisa Mipango Mwandamizi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) Bw. Anthony Rutabanzibwa akitoa somo jinsi waandishi wa habari wanavyotakiwa kuripoti masuala yanayohusu hakiza Binadamu bila kutoka nje maadili ya kazi zao.
Pichani Juu na Chini ni baadhi ya washiriki wakichangia mada na kutoa maoni wakati wa semina hiyo.
Mwenyekiti wa timu ya Mawasiliano ya Umoja Mataifa Bw. Yusuph Al Amin wakati wa semina hiyo akifafanua jinsi sekta ya mawasiliano vikiwemo vyombo vya habari inavyoweza kuchangia maendeleo na kufanikisha kufuatwa kwa haki za binadamu.
Afisa habari wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi.Usia Ledama akitoa changamoto kwa wanahabari kusoma makabrasha yanayotolewa na mashirika mbalimbali ya umoja wa mataifa wakati wa mikutano na semina za kuelimishana kuhusiana na masuala mbalimbali yanayohusu jamii kwani kwa kufanya hivyo ndivyo watakavyoeweza kuelewa ushiriki wa Umoja wa Mataifa katika kupunguza umaskini na kutetea haki za binadamu.
Baadhi ya Maofisa wa Umoja wa Mataifa na Wanahabari wakati wa Semina hiyo.
No comments:
Post a Comment