Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.
Monday, 12 March 2012
Bweni la Wasichana Lawaka Moto Chuo Kikuu Mkwawa
Kikosi cha Zimamoto na polisi wwakizima moto katika bweni la wasichana chuo cha Mkwawa mchana huu Chumba cha wasichana katika chuo cha mkwawa kikiwaka moto Hivi ndivyo moto ulivyoteketeza vyumba viwili katika bweni la wasichana chuo cha Mkwawa Hapa ndipo moto ulipoanzia katika bweni hilo Chumba ambacho moto ulianza kuwaka kikiwa kimeteketea vibaya Mali za wanafunzi zikiwa zimeteketea kwa moto Polisi wakichukua maelezo kwa wahanga wa tukio hilo Mmoja kati ya wahanga akiangua kilio baada ya kufika eneo la tukio na kukuta mali zake zimeteketea kwa moto
Moto mkubwa ambao chanzo chake bado kufahamika umeteketeza vyumba viwili vya bweni la wasichana maarufu kama Hall 6 vyumba Block W katika chuo kikuu kishiriki cha elimu Mkwawa (MUCE) Iringa .
Mashuhuda wa tukio walisema kuwa moto huo ulianza kuwaka katika chumba kimoja wapo chumba Block W muda wa saa 6 mchana na kuwa wakati huo baadhi ya wanafunzi walikuwa wamejipumzisha katika vyumba hivyo .
No comments:
Post a Comment