KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Tuesday, 2 August 2011

FIRST ROUND VODACOM PREMIER LEAGUE FIXTURE 2011/2012, TANZANIA

Magufuli: Barabara za juu zimeanza kujengwa Dar

Serikali imeanza ujenzi wa barabara za juu (flyover), lengo likiwa ni kupunguza msongamano wa magari katika Jiji la Dar es Salaam.
Mpango huo wa kupunguza msongamano huo ambao umekuwa ukisababisha kero kubwa kwa wakazi wa Jiji ulitangazwa na Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, wakati akisoma hotuba ya makadirio ya matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2011/2012.
Waziri Magufuli aliliambia Bunge kuwa usanifu wa barabara ya juu ya Tazara, ulianza Juni mwaka huu kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Japan (Jica). Kadhalika, Dk. Magufuli alisema kuwa serikali imepeleka maombi kwa serikali ya Japan kupitia JICA ili kusaidia ujenzi wa barabara hizo.
BABABARA ZA KUUNGANISHA JIJI
Kwa upande wa barabara za chini, Dk. Magufuli alisema katika mwaka wa fedha huo, serikali itajenga na kukarabati mitandao ya barabara katika Jiji la Dar es Salaam ikiwa ni jitihada za kupunguza msongamano wa magari. Alizitaja barabara zitakazohusika katika mpango huo kuwa ni Ubungo Bus Terminal-Mabibo hadi Kigogo Roundabout yenye urefu wa kilomita 6.4.
Kwa kujibu wa Dk. Magufuli, kazi ya ujenzi wa barabara hiyo inaendelea na utekelezaji wake umefikia asilimia 75.
Dk. Magufuli alisema pia barabara ya Kigogo Roundabout hadi bonde la Msimbazi-Twiga /Msimbazi Junction yenye urefu wa kilomita 2.7 inaendelea kujengwa na utekelezaji wake umefikia asilimia 42.
Waziri Magufuli alisema kuwa barabara nyingine katika mpango huo ni ya Tabata Dampo-Kigogo-Ubungo Maziwa External yenye urefu wa kilomita 2.5 na kuongeza kuwa kazi ya usanifu wa barabara hiyo imekamilika na hatua inayofuata ni kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wake.
Aidha, alisema barabara ya Old Bagamoyo hadi Garden Road yenye urefu wa kilomita 9.1 ipo katika mchakato wa kumpata mhandisi mshauri kwa ajili ya usanifu unaoendelea wakati barabara ya Jet Corner-Vituka-Davis Corner yenye urefu wa kilomita 10.3 kazi ya ujenzi inaendelea.
Dk. Magufuli alisema pia kazi ya usanifu katika barabara za Mbezi (Morogoro Road)- Maramba Mawili-Kinyerezi-Banana yenye urefu wa kilomita 14, Tegeta-Kibaoni-Wazo-Goba-Mbezi Mwisho yenye urefu wa kilomita 20 na Tangi Bovu–Goba yenye urefu wa kilomita 9, imekamilika na kufafanua kuwa hatua inayofuata ni kutafuta fedha kwa ajili ujenzi wa barabara hizo.
Pia alisema kazi ya usanifu inaendelea na itakamilika katika mwaka 2011/2012 kwa barabara za Kimara Baruti-Msewe-Changanyikeni (Km 2.6 ) na Kimara –Kilungule-External Mandela Road (Km 9).
Hali kadhalika, alisema serikali ipo katika mchakato wa kumpata mkandarasi kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Kimara-Magomeni (kilomita 10.4) na Magomeni–Kivukoni, Kawawa (kilomita 10.5), zitakazotumika na Mradi wa Mabasi yaendao Kasi (DART).
KAMATI: MSONGAMANO ATHARI KWA UCHUMI
Kwa upande wake, Kamati ya Bunge ya Miundombinu ilisema kuwa tatizo la msongamano lina athari nyingi kiuchumi na kijamii kwa wakazi wa Dar es Salaam na Taifa kwa ujumla.
Akisoma taarifa ya kamati hiyo, Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Anne Kilango Malecela, alisema wafanyakazi wanachoka kabla ya kuanza kazi kwa kuwa wanatumia muda mwingi barabarani na kuwa hali hiyo imekuwa ikipunguza tija.
Kilango alisema kuwa wastani wa mwendo katika barabara kuu za jiji hilo umefikia kilomita tano hadi 10 kwa saa.
Alisema utafiti uliofanywa na mradi wa DART ulibaini kuwa Tanzania inapoteza Sh. bilioni nne kila siku kutokana na msongamano wa magari katika Jii la Dar es Salaam.
Kamati hiyo ilipendekeza kuwa ili kuondokana na tatizo hilo, mipango yote iliyopendekezwa na wataalam na watafiti mbalimbali itekelezwe.
Aliitaja mipango hiyo kuwa ni kujenga na kuimarisha barabara za michepuo, uboreshaji wa usafiri wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (Uda), kujenga barabara za juu, usafiri wa boti kutoka Bagamoyo mpaka Feri, usafiri wa reli jijini na usafiri wa DART.
WATUMISHI WAKOPESHWE MAGARI
Wakati huo huo, Kamati ya Miundombinu impendekeza kubadili sera ili serikali ibakie na mzigo wa kugharimia magari ya huduma badala ya kugharimia magari yanayotumiwa na maofisa kwenda na kurudi kazini. Akisoma maoni ya kamati hiyo, Kilango alisema katika nchi zinazoendelea watumishi wa serikali wanatumia magari yao na usafiri wa umma kwenda na kurudi kazini.
“Ujenzi wa miradi ya barabara unahitaji fedha nyingi, kwa kuwa serikali haina fedha za kutosha kamati inashauri iangalie maeneo ambayo inaweza kubana matumizi kwa mfano, kupunguza matumizi ya magari yasiyo ya lazima,” alisema Kilango ambaye ni pia ni Mbunge wa Same Mashariki.
Alisema jambo hilo lifanyike kwa kuhakikisha kuwa maofisa wa serikali wanaostahili kutumia magari ya serikali wanakopeshwa magari na kupewa posho maalum kwa ajili ya kununulia mafuta na kuendeshea magari hayo badala ya kutumia magari ya serikali.
Alisema kamati hiyo ilifanya utafiti na kubaini kuwa kwa mwaka wa fedha wa 2011/2012 kiasi cha Sh. 74,637,915,279 zimepangwa kutumika kwa ajili ya kununua mafuta, oil na vilainishi pamoja na kufanya matengenezo ya magari ya serikali.
Aidha, alisema kutokana na aina ya magari yanayotumika na maofisa wengi wa serikali ya Toyota Land Cruiser VX kuwa ya gharama kubwa, serikali inatumia fedha nyingi kwa ajili ya kununua magari hayo ikiwa ni wastani wa Sh. 260,000,000 kwa gari moja ambalo hutumiwa na ofisa mmoja tu.
UPINZANI: MASHANGINGI YAPIGWE MNADA
Kwa upande wake, kambi ya upinzani ikiwasilisha bajeti yake mbadala, ilitaka magari ya kifahari yanayotumiwa na viongozi na watumishi wa umma yauzwe kwa mnada ndani ya miezi sita na viongozi hao wakopeshwe magari kwa ajili ya kutekeleza majukumu yao mbalimbali.
Msemaji wa Kambi ya Upinzani wa Wizara ya Ujenzi, Salvatory Machemli, aliitaka serikali kuandaa utaratibu utakaowawezesha viongozi na watendaji kupata usafiri wa gharama nafuu badala ya utaratibu uliopo.
SENDEKA ALALAMIKIA FEDHA ZA BARABARA
Mbunge wa Simanjiro (CCM), Christopher Ole Sendeka, amelalamikia mgawanyo wa fedha za ujenzi wa barabara akisema serikali inayoelekea kufa, kila mmoja hunyofoa kitu chake.
“Siku zote serikali iliyoanza safari ya kifo ni kila mmoja kunyofoa kitu chake,” alisema Ole Sendeka wakati alipoomba mwongozo wa Mwenyekiti bungeni jana.
Mbunge huyo alitaka bajeti ya Wizara ya Ujenzi, ifumuliwe kwa kuwa haikuzingatia usawa, bali imejaa upendeleo wa maeneo yanayotoka viongozi.
Akizungumza mara baada ya kupewa ruhusa na Mwenyekiti wa Bunge, George Simbachawene, alisema upendeleo uliopo katika miradi ya barabara ni dalili mbaya kwa serikali. Alisema kuna barabara kadhaa zikiwemo za Mkoa wa Kilimanjaro, na kuzitaja barabara ya Sadala-Masama iliyotengewa fedha kwa ujenzi wa kiwango cha lami, barabara ya Kibosho Shine-Kwa Raphael, Rau-Madukani hadi Mawela Uru, Kwa Nduoni na nyingine ni ile ya Tarakea Rongai hadi Kamwanga.
“Huu ni mgawanyo wa rasilimali usio na uwiano sawa, inafika hali hii kila mtu anataka kunyofoa kipande chake, serikali inatakiwa kuwa makini,” alisema.
Alisema cha kusikitisha ni kwamba katika ujenzi wa barabara ya Kia kwenda Mererani ilitengewa fedha katika bajeti ya mwaka wa fedha wa 2010/2011 haikutekelezwa na pia haimo katika bajeti ya Wizara ya Ujenzi iliyosomwa jana bungeni. Akijibu mwongozo huo, Simbachawene alisema kuwa jambo hilo ni zito hivyo mwongozo utatolewa leo.

CCM gives Lowassa, Chenge a month to resign

CCM Ideology and Publicity Secretary Nape Nnauye briefs the media in Dodoma yesterday on resolutions made by the ruling party�s Central Committee at its meeting held in the municipality at the weekend.
Two sitting Members of Parliament, both prominent members of the ruling CCM and former cabinet ministers, have been given until next month to relinquish their positions in the party or risk being shown the door.
Former Prime Minister Edward Lowassa and former Attorney General Andrew Chenge are associated – alongside businessman Rostam Aziz – with controversial transactions that have cost the country dearly financially and in various other ways as well as tainted the party’s image.
However, Aziz has since heeded calls by the party that he give way by recently resigning as member of the powerful CCM National Executive Committee (NEC) and as MP for Igunga constituency in Tabora Region.
The deadline just given is among the resolutions made here by the party’s Central Committee (CC) that also set the date for the next sitting of the NEC, the body empowered to take measures in line with the decision reached in April this year in connection with the matter.
At its April meeting, also held here, the committee resolved that all CCM leaders associated with corrupt practices resign from all party’s positions, failure which the party would act hard against them.
“NEC will meet again sometime in September where, among other things, it will evaluate the progress made in implementing previous decisions,” CCM Ideology and Publicity Secretary Nape Nnauye declared at a media briefing at the end of the CC meeting yesterday. “The party is determined to ensure that the party cultivates and promotes ethical practice within all its ranks and calls upon all those ordered to resign to use the time available to act accordingly in the party’s interest,” he said.
Commenting on widely circulating reports that CCM was reluctant to take measures against beleaguered bigwigs Lowassa and Chenge for fear that their popularity among MPs would see the party disintegrate, Nnauye said: “‘No individual within CCM is more famous, popular or important than CCM itself. CCM is not worried about or scared of anything or anyone. It’s much better that we lose a constituency or a ward in a by-election than continue embracing unethical leaders.”
He brushed aside “any possibility” of the party standing on dangerously shaky ground by taking the decisions it was taking, noting: “Let all those thinking or believing that they can lure CCM members to defect proceed with their plans. We once had strong leaders such as (former minister) Augustine Mrema and (former Zanzibar Chief Minister) Seif Shariff Hamad and they defected, yet CCM has weathered the storms and remained unshaken.”
Reacting to the trio’s pronouncements to the effect that NEC has never directed that they resign, as repeatedly reiterated by members of the party’s secretariat leaders, Nnauye said information on all resolutions is always relayed during formal meetings “and there was no way they can be altered at random”.
Lowassa resigned as PM in February 2008 after being associated with involvement in a controversially awarded tender for emergency power generation to Richmond Company, which had no capacity to deliver. He however, remains a NEC member and legislator for Monduli.
Chenge, who similarly still sits on the NEC and is MP for Bariadi West, is said to have benefited financially from the 1999 controversial purchase of radar from the UK at a cost of 40 million sterling pounds instead of the market value of around 12 million pounds. He resigned as Infrastructure minister in 2008 following intense pressure from the public.
Rostam Aziz is said to be closely connected to the company which many believe contributed to Lowassa’s fall from grace. This is none other than Kagoda Agricultural Ltd, one of the firms that benefited from the 133 billion/- suspiciously withdrawn from the Bank of Tanzania’s External Payment Arrears (EPA) account in 2005.
The trio’s suspicious practices and behaviour are widely believed to have contributed to CCM’s relatively poor performance in the October 2010 General Elections that saw eventual presidential poll winner Jakaya Kikwete to garner a mere 61 per cent of the total vote compared to 80 per cent in 2005.
CCM also suffered massive defeats in key urban constituencies in Mwanza, Mbeya, Arusha, Iringa and Dar es Salaam regions. The Opposition camp shone in some traditionally CCM strongholds in the rural parts of Shinyanga, Mwanza, Kigoma, Mbeya and Arusha regions.
Unlike Lowassa and Chenge, who have yet to heed CCM’s resignation orders, Rostam Aziz announced his resignation from the NEC and as MP on July 13.
Nnauye said CCM will soon draw up a timetable that would lead to the announcement of the party’s flag bearer in the Igunga by-election.
“CCM has received and accepted Aziz’s decision to relinquish his posts in the party and as an MP and has resolved that all campaign-related activities will be conducted under the leadership of our Tabora regional and Igunga district offices. We are confident that we will retain the constituency,” he added.

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dk Asha-Rose Migiro Amtembelea Rais Wa Zanzibar Dk Ali Shein

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akibadilishana mawazo na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dk Asha Rose Migiro,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dk Asha Rose Migiro,alipofika Ikulu Mjini
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akizungumza na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dk Asha Rose Migiro,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar.02/08/2011.Picha na Ramadhani Othamn, Ikulu-Zanziba

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA KILIMO CHA ZABIBU DODOMA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia wakulima wa Zabibu baada ya kutembelea na kukagua mashamba, wakati alipowasili Kijiji  cha Chilangali (2) Wilaya ya Chamwino Mkoa wa Dodoma leo Agosti 02, 2011 kukagua mradi wa kilimo cha Zabibu (FUNE) katika shamba hilo lenye ukubwa wa Hekari 300.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe, wakiangalia Pikipiki aina ya Bajaj, aliyoizindua na kumkabidhi Mwenyekiti wa SACCOS ya FUNE, Jones Mazengo. Bajaj hiyo imetolewa na Benki ya CRDB ili itumike katika shughuli za kutembelea shamba la Mizabibu lililopo kijijini Chilangali (ii), likiwa na hekari 300 ambazo zinamilikiwa na wananchi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi funguo ya Bajaj, Mwenyekiti wa SACCOS ya FUNE, Jones Mazengo baada ya kuzindua rasmi leo Agosti 02, Bajaji hiyo iliyotolewa msaada na Benki ya CRDB kwa ajili ya kutumika kwa shughuli za kutembelea shamba la Mizzabibu lililopo kijiji cha Chilangali (ii) Wilaya ya Chamwino mkoa wa Dodoma, likiwa na ukubwa wa hekari 300.Katikati ni Mama Asha Bilal.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Asha Bilal, wakisikiliza maelezo kutoka kwa mwendeshaji wa mitambo ya kusukumia maji kwenda katika mashamba ya Zabibu, Aloyce Zakaria,  wakati walipofika Kijiji  cha Chilangali (ii) Wilaya ya Chamwino Mkoa wa Dodoma leo Agosti 02, 2011 kukagua mradi wa kilimo cha Zabibu (FUNE) katika shamba hilo lenye ukubwa wa hekari 300.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na mkewe Mama Asha Bilal, wakifurahia ngoma ya asili kabira la Wagogo, wakati walipowasili Kijiji  cha Chilangali (ii) Wilaya ya Chamwino Mkoa wa Dodoma leo Agosti 02, 2011 kukagua mradi wa kilimo cha Zabibu (FUNE) katika shamba hilo lenye ukubwa wa Hekari 300.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Asha Bilal, wakikagua miche ya mizabibu, wakati walipowasili Kijiji  cha Chilangali (ii), Wilaya ya Chamwino Mkoa wa Dodoma leo Agosti 02, 2011 kukagua mradi wa kilimo cha Zabibu (FUNE) katika shamba hilo lenye ukubwa wa hekari 300.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe, Mama Asha Bilal,  wakisikiliza maelezo ya Mkulima wa Zabibu, Gulavile Chikamanjenzi (kulia) wakati walipowasili Kijiji  cha Chilangali (ii) Wilaya ya Chamwino Mkoa wa Dodoma leo Agosti 02, 2011 kukagua mradi wa kilimo cha Zabibu (FUNE) katika shamba hilo lenye ukubwa wa hekari 300.
Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikagua moja ya bomba linalopitisha maji kwenda katika miche ya mizabibu  wakati walipowasili Kijiji  cha Chilangali (ii) Wilaya ya Chamwino Mkoa wa Dodoma leo Agosti 02, 2011 kukagua mradi wa kilimo cha Zabibu (FUNE) katika shamba hilo lenye ukubwa wa Hekari 300. Kulia ni mmoja kati ya wakulima wa mashamba hayo, Gulavile Chikamanjenzi, akimpa maelezo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Asha Bilal, wakiangalia Valve ya kuruhus maji kwenda mashambani ,  wakati walipofika Kijiji  cha Chilangali (ii) Wilaya ya Chamwino Mkoa wa Dodoma leo Agosti 02, 2011 kukagua mradi wa kilimo cha Zabibu (FUNE) katika shamba hilo lenye ukubwa wa hekari 300.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe, Mama Asha Bilal, wakiangalia Bwawa la kuhifadhia maji ya kumwagilia mashamba ya Zabibu, wakati walipowasili Kijiji  cha Chilangali (ii) Wilaya ya Chamwino Mkoa wa Dodoma leo Agosti 02, 2011 kukagua mradi wa kilimo cha Zabibu (FUNE) katika shamba hilo lenye ukubwa wa Hekari 300.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe, Mama Asha Bilal, wakitoka kukagua mashamba ya zabibu, wakati walipowasili Kijiji  cha Chilangali (ii) Wilaya ya Chamwino Mkoa wa Dodoma leo Agosti 02, 2011 kukagua mradi wa kilimo cha Zabibu (FUNE) katika shamba hilo lenye ukubwa wa hekari 300. Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi Ya Makamu Wa Rais