KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Tuesday, 2 August 2011

MO DEWJI AWAHIMIZA WALIMU JIMBONI MWAKE KUFANYAKAZI KWA BIDII ILI KUONDOA AIBU YA MATOKEO YA MITIHANI JIMBONI KWAKE

Mbunge Dewji akizungumza na walimu wa sekondari.Wa pili kulia ni makamu mwenyekiti wa manispaa ya Singida,Pantaleo Sorongai na anayefuata ni Msitahiki meya wa manispaa ya Singida,diwani wa kata ya Majengo na Sheikh wa mkoa wa Singida,Salimu Mahami.Wa kwanza kulia aliyeshika mdomo,afisa elimu sekondari manispaa ya Singida,Magreth Mafita.
Makamu mwenyekiti wa manispaa ya Singida na diwani wa kata ya Mitunduruni,Pantaleo Sorogai,akisalimia walimu wa sekondari za manispaa ya Singida.Wa kwanza kushoto ni mbunge Dewji,kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Singida,Hoja,afisa elimu sekondari manispaa ya Singida,Magreth Mafita na katibu wa CWT mkoa,Ismael.
Afisa elimu sekondari manispaa ya Singida,Magreth Mafita akitoa taarifa yake kwa mbunge wa jimbo la Singida mjini,Mohammed Dewji.Wa kwanza kushoto,Meya wa manispaa,Sheikh Salum Mahami na kulia,kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Singida,Hoja.
Mbunge wa jimbo la Singida mjini Mohammed Dewji (katikati).Kushoto makamu mwenyekiti wa manispaa ya Singida na diwani wa kata ya Unyankindi,Pantaleo Sorongai,kulia aliyeshika mdomo ni afisa elimu sekondari manispaa ya Singia,Magreth Mafita.
walimu wa shule za sekondari za manispaa ya Singida.
---
Na.Mwandishi wetu.

Walimu wa shule za sekondari jimbo la Singida mjini, wamehimizwa kukaza ‘buti’ katika kutekeleza wajibu wao, ili kuinua taaluma itakayowawezesha wanafunzi kuondokana na aibu ya matokeo mabaya ya mtihani wa kidato cha pili na ule wa kidato cha nne.

 Changamoto hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki  na mbunge wa jimbo hilo, Mohammed Gullam Dewji, wakati akizungumza kwenye kikao cha pamoja na walimu wa shule 20 za sekondari za manispaa ya Singida.

 Aliwaomba waendelee na moyo wao huo wa kujituma kwenye kazi yao ya ufundishaji, ili kunyanyua ufaulu wa wanafunzi.

“Taarifa nilizo nazo, hali ya ufaulu kwenye shule zetu iko chini mno, ni imani yangu kuwa baada ya kikao chetu  hiki, morari na juhudi za ufundishaji mtaziendeleza kwa ari zaidi, nguvu zaidi na kasi zaidi” alifafanua.

 Aidha, Dewji ambaye pia ni mjumbe wa MNEC wa mkoa wa Singida,aliwataka waendelee kuwa wavumilivu wakati huu ambao serikali inaendelea kutatua changamoto nyingi zinazowakabili katika utekelezaji wa majukumu yao.

 “Changamoto mlizoziwasilisha kwangu, tutajipanga mimi na viongozi wenzangu tuone ni kwa jinsi gani tunaweza kuzitatua zile zilizo ndani ya uwezo wetu, na zile ambazo ziko nje ya uwezo wetu, tutaziwalisha serikalini kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi wa kudumu”,alisema.

 Awali afisa elimu wa shule za sekondari katika manispaa ya Singida, Magreth Mafita, alitaja baadhi ya changamoto zinazoikabili ofisi yake, kuwa ni kucheleweshwa kulipwa kwa madai ya walimu na uhaba mkubwa wa walimu.

 Mafita alitaja changamoto zingine kuwa ni uhaba wa vyumba vya madarasa, shule mpya kutokuwa na barabara za kuziunganisha na sehemu zingine na ufaulu usioridhisha wa asilimia 42.

 “Hata hivyo, mheshimiwa mbunge naomba nitumie fursa hii kukupongeza sana kwa juhudi zako za dhati zilizopelekea jimbo la Singida mjini, kuwa na shule za sekondari za serikali 17 kati ya mbili zilizokuwepo mwaka 2005”,alisema afisa huyo na kushangiliwa kwa nguvu na umati wa walimu.

MWISHO

Plastic heart gives dad Matthew Green new lease of life


Matthew Green with his wife Gill and son Dylan 
Mr Green says he is excited about playing in the garden with his son
A 40-year-old father who was dying from heart failure is set to leave hospital after receiving an artificial heart.
Matthew Green is ready to go home and await a transplant after surgeons at Papworth Hospital in Cambridgeshire replaced his heart with an implant.
His new plastic heart is powered by a portable driver in a backpack, which he said had "revolutionised" his life.
It is thought to be the first time a UK patient has been able to go home with an entirely artificial heart.
Around 900 similar operations have been carried out around the world.
Mr Green said: "It's going to revolutionise my life. Before I couldn't walk anywhere. I could hardly climb a flight of stairs and now I've been up and I've been walking out and getting back to a normal life.
"I went out for a pub lunch over the weekend and that just felt fantastic, to be with normal people again."
Consultant cardiothoracic surgeon Mr Steven Tsui said without the device Mr Green, from London, might not have survived the wait for a heart transplant operation.
"At any point in time there may be as many as 30 people waiting for a heart transplant on our waiting list at Papworth, with one third waiting over a year," he said.

'Excellent recovery'
The BBC's David Shukman explains how the artificial heart works

"Matthew's condition was deteriorating rapidly and we discussed with him the possibility of receiving this device, because without it, he may not have survived the wait until a suitable donor heart could be found for him."
He said for the first time a patient was walking the streets of Britain without a human heart.
Mr Green, who is married and has a son, had been suffering from Arrhythmogenic Right Ventricular Cardiomyopathy (ARVC), a heart muscle disease that results in arrhythmia, heart failure and occasionally sudden death.
His health had declined over recent years, meaning the only option available to him was a heart transplant.
Earlier, he thanked the Papworth staff for making "it possible for me to return home to my family".
"Two years ago I was cycling nine miles to work and nine miles back every day, but by the time I was admitted to hospital I was struggling to walk even a few yards," he said.
"I am really excited about going home and just being able to do the everyday things that I haven't been able to do for such a long time, such as playing in the garden with my son and cooking a meal for my family."
The SynCardia temporary Total Artificial Heart Mr Green received is used as a bridge-to-transplant for patients dying from end-stage biventricular heart failure, where both sides of the heart are failing.
The device works in the same way as a heart transplant in that it replaces both failing ventricles and the heart valves they contain, thus relieving the symptoms and effects of severe heart failure. However, it is not suitable for long-term use.
Mr Tsui, director of the transplant service at Papworth, said the operation on 9 June "went extremely well".
"Matthew has made an excellent recovery," he said.
"I expect him to go home very soon, being able to do a lot more than before the operation - with a vastly improved quality of life - until we can find a suitable donor heart for him to have a heart transplant."
Mr Green will leave Papworth with a backpack containing a 13.5lb (6kg) portable driver to power his new heart.
Papworth Hospital carries out 2,000 major heart operations a year - more than any other hospital in the UK. Its first heart transplant, in 1979, was a UK first and the hospital has been using mechanical devices to support patients with end-stage heart failure since the 1980s.
The Total Artificial Heart is a modern version of the Jarvik-7 artificial heart of the 1980s. In November, 1986, a patient received a Jarvik heart and was supported for two days before receiving a transplant.
It is understood that other patients with mechanical hearts have been sent home before, but never with both ventricles replaced.
Health Secretary Andrew Lansley said: "The NHS has a long and proud track record of innovation that has driven major improvements in patient care in the past.
"The success of this procedure at Papworth Hospital is an excellent example of how the NHS can continue to provide the best treatment and outcomes for its patients in the future."
Professor Peter Weissberg, medical director at the British Heart Foundation, said that for some patients, with severe heart failure, transplantation is their only hope of long-term survival, but donor hearts are not always available.
He added: "Patients with mechanical hearts must remain permanently linked to a power supply via tubes that pass through the skin, which is a potential source of infection.
"With this artificial heart, the power supply is small enough to fit in a shoulder bag so patients can walk around and go home."

Monday, 1 August 2011

MH BALOZI MAAJAR AONGEA NA MABLOGA WA DMV



Mh,Balozi Mwanaidi Maajar akiongea na Bloggers wa DMV akiwaelezea kuhusu matayarisho ya Miaka 50 ya Uhuru na mkutano wa DICOTA na kuwaomba BLOGGERS wote Marekani wasaidie kusambaza habari za sherhe hizi za Uhuru na mkutano wa DICOTA zitakazofanyika Sep 22-25,2011 Marriott Hotel iliyopo DULLES AIRPORT pia maeomba Watanzania wote Marekani wajiandikishe kwa wingi na anaomba kama inawezekana uchukue likizo mapema kusudi uwepo Washington,DC kuanzia alhamisi ya Sep 22,2011,kwani Miaka 50 ya Uhuru si kitu kidogoAfisa Ubalozi Suleiman Saleh akichangia katika mkutano huo wa Bloggers wa DMVKulia ni Blogger Mubelwa Bandio(www.changamotoyetu.blogspot.com) akiwa makini kumsikiliza Mh.Balozi Mwanaidi Maajar na shoto ni afisa Ubalozi,Suleiman Saleh.Blogger Sunday Shomari(www.sundayshomari.com)akifurahia majibu mazuri kutoka kwa Mh.Balozi Mwanaidi maajar(hayupo pichani) baada ya kumuuliza swali.Mh.Balozi Mwanaidi Maajar(wa pili kutoka shoto) akiongea na Blogger DMV,wa pili toka kulia ni afisa Ubalozi Suleiman Saleh,shoto ni Sunday Shomari na kulia ni Mubelwa Bandio Picha kwa hisani ya www.issmichuziblogspot.com

Tangazo La Kufturu Jijini Stockholm




Waislam pamoja na marafiki zao mnatangazia kujumuika kwa pamoja kuja kufturu siku ya Tarehe 6.13.20 na 27 Mahali Hagsätra..Tafadhalini mnaomba tujitahidi kuhudhuria
KINA BABA NA KINA MAMA.
Kwa mawasiliano zaidi tembelea (chafosa@yahoo.com
JAZAKAL LAH KHAYR 

Watu 242 wauawa kwa ushirikina Shinyanga


Watu 242 wameuawa mkoani hapa kwa imani za kishirikina katika kipindi cha januari 2010 hadi juni mwaka huu.
Kamanda wa Polisi wa mkoani Shinyanga, Diwani Athumani, aliwambia wadau wa ulinzi shirikishi kuwa matukio hayo yamekithiri hasa katika kipindi cha Januari hadi Juni mwaka huu.
Akitoa taarifa yake mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dk. Yohana Balele, na wadau wa jeshi hilo mkoani hapa, Kamanda huyo alisema katika kipindi cha Januari hadi Desemba 2010, watu waliouawa kwa imani hizo ni 63.
Kamanda huyo aliongeza kuwa katika kipindi cha kuanzia Juanuri hadi Juni mwaka huu, watu 36 waliuawa ikilinganishwa na watu 18 mwaka 2010 ambao ni ongezeko la watu 18 na sawa na asilimia 100 ya ongezeko la mauaji ya aina hiyo.Alisema watu 45 waliuawa katika kipindi cha Januari hadi Juni mwaka huu ikilinganishwa na watu 29 waliouawa katika kipindi kama hicho mwaka 2010 na kuwepo kwa ongezeko la watu 16 sawa na asilimia 55.
Kutokana na hali hiyo, alisema jeshi hilo limejipanga na kuweka mikakati ya kuhakikisha kuwa mauaji hayo yanapungua kama si kukoma kwa kutumia moja ya mbinu zake za kuielimisha jamii na kuihamasisha kuacha mauaji hayo.
Kwa upande wake, Balele, alikemea tabia ya wakazi wa Mkoa wa Shinyanga ya kujichukulia sheria mkononi na kuwaua watu wasiokuwa na hatia.
Takwimu za mauaji hayo zinaonyesha kuwa Wilaya ya Bariadi ndiyo inayongoza kwa mauaji ikifuatiwa na Bukombe na Kahama huku Maswa na Manispaa ya Shinyanga zikiwa na idadi ndogo.

Stars` bumpy road to 2014 World Cup


Taifa Stars
Tanzania national soccer team, the Taifa Stars have a troubled route to win the 2014 World Cup to be hosted by Brazil for the second time in history since 1950.
The Tanzania team has been pushed to join group C that has formidable and regular campaigners Cote d’Ivoire, Morocco and Gambia.
However, the Stars group C inclusion is not automatic as the team need to knockout Chad in the prequalification tie to be played in November.
While eliminating Chad will not be an easy task, Stars’ progression into the finals berth might be another daunting task as well.
The World Cup draw conducted at the Rio de Janeiro’s Copa Cabana beach
under FIFA general secretary Jerome Valcke came as a shock to most of the fans in Tanzania.
The World 2014 qualifiers looks to be the toughest ever for the country that has never managed to play in the finals since attaining independence 50 years ago.
Despite efforts by the Government and the football federation in the country, Stars are still handing in triple digit figures of the FIFA rankings to cast doubt of the team’s ability to sail through the qualifiers.
Should Stars manage to kick out Chad, then the team has to prepare for the group stage qualifiers that get underway
on June 1 next year up to September 10 2013.
Tanzania ranked 127 against Chad’s 158 looks to be an easy task but football is not always about rankings.
Only Mauritania that has been excluded in the race towards the 2014 World cup qualifiers out of the 53 FIFA members from the continent.
Top ten teams in the continent have been leading the seeding for the qualifier groups and these are South Africa, Tunisia, Cote d’Ivoire, Ghana, Burkina Faso, Nigeria, Egypt, Algeria, Cameroon and Senegal.
Africa has five slots in the World Cup which will be competed by 32 nations including hosts Brazil that have won the title for a record five times since its inauguration in 1930.
Despite huge efforts by the Government to lift the standard of the game through footing bills of the senior and youth national team coaches, still Stars are far from making impact at high profile competitive soccer.

Chadema youth wing faults AG over `plan` to restrict demos

By Devota Mwachang`a

Chadema Youth Council National Chairman John Heche (R) with the council`s chairman for Mbeya Region, Emmanuel Mwakajila, at a news conference in Dar es Salaam yesterday.
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) youth council (Bavicha) yesterday challenged attorney general (AG) Fredrick Werema’s remarks that the government would amend a law on demonstrations.
Addressing a press conference in Dar es Salaam yesterday Bavicha chairman John Heche said the move was intended to stop his party from conveying its message to the people.
He explained that Chadema’s demonstrations across the country helped the party to get its message across on issues that hindered the country’s development.
He mentioned some of the issues which had been addressed by the party during demonstrations as the power crisis, the high costs of living, illegal demolitions, human rights and depletion of national resources like minerals.
“The demonstrations have prompted the government to reduce sthe ugar price which was very high in previous months,” he said adding that Chadema would continue with its peaceful demonstrations.
The Bavicha chairman said he was taken aback by the AG’s remarks on the government’s intention to introduce the law limiting demonstrations while there were many bad laws which needed urgent amendments but the government ignored them.
He explained that the government would be denying people their constitutional rights if it restricted peaceful demonstrations as that would contravene the right to freedom of expression and association.
Heche noted that Chadema planned to organise another demonstration if the government continued with its plans to restrict peaceful demonstrations which raised public awareness.
Meanwhile, the Bavicha chairman told Deputy Speaker Job Ndugai and Chama Cha Mapinduzi MPs to be careful while making decisions in the National Assembly because they were lowering its credibility.

Zombe amlipua Lema


James Magai

MKUU wa Upelelezi wa zamani wa Mkoa wa Dar es Salaam,Abdallah  Zombe ameibuka tena na kutoa kali kwa kudai kuwa siku Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kikiingia madarakani yeye atajinyonga.

Zombe ambaye alishinda kesi ya mauaji, iliyokuwa ikimkabili yeye na askari wengine 12, alitoa kali hiyo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari nje ya Mahakama Kuu Dar es Salaam kufuatia hotuba ya chama hicho bungeni kuhoji kuachiwa kwake.

Katika kesi hiyo iliyovuma tangu walipokamatwa mwaka 2006, walikuwa wakituhumiwa kuwaua kwa makusudi wafanyabiashara wanne wa madini Kutoka Mahenge na dereva teksi wa Manzese Dar es Salaam, katika msitu wa Pande wilayani Kinondoni nje ya Jiji la Dar es Salaam.
Walikuwa wakituhumiwa kuwaua Sabinus Chigumbi maarufu kama Jongo, Ephrahim Chigumbi, Mathias Lunkombe na dereva teksi Juma Ndugu wa Manzese Dar es Salaam.

Hata hivyo Agosti 17, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam iliwaachia huru baada ya Jaji wa Mahakama ya Rufani Salum Masatti aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo kuridhika kuwa hakuna ushahidi wa kuwatia hatiani kwa mashtaka yaliyokuwa yakiwakabili.
Lakini Julai 28, mwaka huu, Waziri kivuli wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Mbunge wa Arusha  Mjini, Godbless Lema  alihoji sababu za kuachiwa kwa Zombe na wenzake.

Katika hotuba yake bungeni mwishoni mwa wiki, Lema alihoji kuachiwa kwa Zombe na wenzake wakati akisoma hotuba ya kambi ya Upinzani, baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha kuwasilisha bajeti ya wizara yake hiyo.Hatua hiyo ya Chadema kuhoji kuachiwa kwake ilimkera Zombe ambapo jana alizungumza na waandishi wa habari na kuelezea kushangazwa na hatua hiyo ya Chadema kuhoji bungeni mamlaka ya mahakama.

Zombe alisema kuwa ni dhahiri kuwa wabunge wa chama hicho hawajui majukumu yao kama wabunge wala sheria na Katiba ya nchi licha ya kuapa kuilinda Katiba hiyo na kwamba ndio maana wanafanya mambo ya kitoto bungeni.

Aliongeza kuwa kutokana hali hiyo hawafai kupewa nchi kuiongoza na akatamka kuwa siku wakiongoza nchi yeye atajinyonga.  “Julai 28 mwaka huu nilishangaa sana sana na kauli ya mbunge aliyeonyesha kutokujua taratibu za sheria za nchi hii;
Baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha kumaliza kuwasilisha bajeti ya wizara yake, Godbless Lema mbunge wa Chadema akiwa waziri kivuli wa wizara hiyo, wadhifa ambao nadhani hastahili kuwa nao aliuliza swali kuwa ni kwa nini Zombe aliachiwa”, alisema.

Alisema  “Ile hotuba sijui ilitengenezwa na nani lakini huyu ni mtu hatari sana maana haijui kabisa Katiba,” alisisitiza Zombe, huku akinukuu Ibara ya 107 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano inayosema kuwa chombo chenye mamlaka ya mwisho katika kutoa haki ni mahakama.

“Mbunge anahoji uamuzi ya mahakama bungeni, kwanza uamuzi ule haujui, hajawahi kuusoma kujua Zombe amedhulumiwa haki zake kiasi gani;
“Anapaswa kujua mgawanyo wa madaraka wa mihimili ya dola ambayo ni Serikali Bunge na Mahakama.Mbunge hawezi kuingilia maamuzi ya mahakama. Mahakama iliamua Zombe aachiwe wewe unahoji ameachiwaje?” alisema huku akionyesha kukerwa.

Hata hivyo, Zombe alisema kuwa kama angehoji kuhusu askari wengine walioua raia ni kwanini hawajafikishwa mahakamani ingekuwa ni sahihi lakini si kuhoji uamuzi wa mahakama.Akizungumza kuhusu kesi aliyoifungulia Serikali  akiidai Sh5.2bilioni alisema  inatarajiwa kuanza kusikilizwa Septemba 8, 2011, mbele ya Jaji Upendo Msuya.

 Lema ajibu

Naye Lema alipoulizwa jana mjini Dodoma  alisema hotuba ile yeye aliitoa bungeni na hivyo hawezi kujibizana na Zombe bali anaweza kujibizana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.Lema alisisitiza kuwa Zombe alikuwa ni mtuhumiwa wa mauaji ya raia na kwamba mahakama kumwachia huru haina maana kwamba hakuwa na kosa.“Huyu si saizi yangu, yeye ni mtuhumiwa tu na mimi sina tuhuma yoyote katika kituo chohote cha polisi kuhusu tuhuma hizo.

Shule Ya Msingi Mchuchuma, Ludewa Ina Walimu Wawili Tu


Mwalimu Mkuu msaidizi  wa shule ya Msingi Mchuchuma, wilaya ya Ludewa, mkoani Iringa Bw.Joseph Thomas Lugome (58), akionyesha darasa la saba ambalo limekuwa likisomewa pia  na  wanafunzi  wa darasa la sita kwa kupokezana na darasa la saba  kutokana na shule  hiyo yenye  wanafunzi zaidi ya 200 kuwa na  walimu  wawili pekee. 
                    SHULE ya msingi Mchuchuma katika wilaya ya Ludewa mkoani Iringa yenye wanafunzi 208 wakiwemo wanafunzi wasichana 90 na wavulana 118 imekuwa ikifundishwa na mkuu wa shule na makamu mkuu wa shule pekee ambao wote ni wanaume .


Uchunguzi uliofanywa na timu ya waandishi wa habari za mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP ) mkoani Iringa umebaini kuwepo kwa hali hiyo ambayo pia imekuwa ikiwapa wakati mgumu walimu hao hasa pindi wanafunzi wa kike wanapougua na kuhitaji msaada wa kupelekwa katika matibabu .
  Hata hivyo kutokana na upungufu mkubwa wa walimu katika shule hiyo ambayo inaelezwa kujengwa juu ya madini ya mchuchuma na linganga ,umekuwa ukikwamisha kwa kiasi kikubwa ufaulu wa wanafunzi katika shule hiyo na kupelekea baadhi ya watoto kuacha shule kwa kutokana na kukosa walimu wa kuwafundisha .
   Mmoja kati ya wazazi wa wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo Augustino Haule alisema kuwa kwa upande wake alikuwa na watoto wawili waliokuwa wakisoma katika shule hiyo ila mmoja wa kike ambaye alikuwa darasa la saba amelazimika kumwachisha shule baada ya muda mwingi kushida mitaani baada ya walimu kutofundisha mara kwa mara.
  Haule alisema kuwa mbali ya walimu kuwa wachache katika shule hiyo ila bado mazingira ya shule hiyo yamekuwa yakichangia watoto kuacha shule kutokana na muda mwingi kufanya kazi za kupika na kuchota maji ya walimu umbali wa zaidi ya kilomita 2 kutoka katika shule hiyo.
  Pia alisema kuwa ni vema serikali kuifunga kabisa shule hiyo hadi pale itakapolipatia ufumbuzi tatizo la upungufu wa walimu kuliko serikali kuendelea kuwaacha wanafunzi zaidi ya 200 kufundishwa na walimu wawili pekee tena wote wakiwa ni wanaume.
 Mwalimu mkuu mssaidizi wa shule hiyo Joseph Lugome alithibitisha uhaba huo wa walimu katika shule hiyo na kuwa hadi sasa kwa zaidi ya wiki mbili mwalimu amebaki peke yake baada ya mwenzake kupata matatizo ya kiafya.
 Alisema kuwa katika shule hiyo wanafunzi 47 ni darasa la saba ambao wanangoja kufanya mtihani wa Taifa wa kuhitimu elimu ya msingi na kati ya wanafunzi hao wasichana ni 24 na wavulana ni 25 huku wanafunzi wa darasa la nne katika shule hiyo ni 10 pekee wasichana wakiwa 11 na wavulana 8.
 Hata hivyo alisema kuwa kutokana na shule hiyo kutokuwa na maji wanafunzi wamekuwa wakipagiwa zamu ya kuchota maji ya walimu umbali wa kilomita zaidi ya 2 kutoka katika shule hiyo ili kutoka nafasi ya walimu kufundisha wanafunzi wengine .
 Kwani alisema kuwa iwapo walimu wataondoka na kwenda kutafuta maji basi upo uwezekano wa wanafunzi kuendelea kukosa vipindi .
 Lugome alisema kuwa wakati mwingine shule hiyo imekuwa ikifungwa kwa muda iwapo wanafunzi zaidi ya mmoja wataugua na walimu hao kufanya kazi ya kuwabeba mgongoni wanafunzi hao wagonjwa na kuwapeleka zahanati iliyopo kijiji cha jirani kilichopo umbali wa zaidi ya kilometa zaidi ya 12 kijiji cha Nkomang'ombe.
 Pamoja na mazingira hayo ya kufundisha yakiwa magumu bado mwaka jana shule hiyo darasa la saba ambalo lilikuwa na wanafunzi 36 wanafunzi 8 walifaulu kujiunga na elimu ya sekondari.
  Aidha alisema kuwa mbinu za ufundishaji ambazo zimekuwa zikitumiwa katika shule hiyo yenye walimu wawili ni pamoja na kuunganisha madarasa kwa kufanya darasa la kwanza na la pili ndani ya chumba kimoja na darasa la tatu na la nne kuwa ndani ya darasa moja na darasa la sita wamekuwa wakisoma kwa kupokezana na wale wa darasa la saba.
  Mwalimu Lugome alisema kuwa tatizo la utoro kwa wanafunzi limekuwa ni sugu kwa kipindi cha masika zaidi kutokana na wanafunzi kutoka mbali na shule hiyo umbali wa zaidi ya kilomita 2 na kuwa kutokana na mvua na mito kujaa maji wa wanafunzi ambao wamekuwa wakifika shule ni 100 ama 90 pekee na sehemu kubwa hushindwa kufika shule.
  Afisa elimu wa wilaya ya Ludewa Robart Hyella amethibitisha kuwepo kwa tatizo la uhaba wa walimu katika shule za msingi ndani ya wilaya hiyo na kuwa shule zinazoongoza kwa upungufu wa walimu ni zile za pembezoni mwa wilaya hiyo . Imeandikwa na Francis Godwin(TGNP),Ludewa

Music therapy may help depression

musical score  

Does music have a role in treating depression?
Music therapy can be used to improve treatment of depression, at least in the short term, say researchers in Finland.
The technique used non-verbal communication to help patients express their emotions.
A study on 79 people, published in the British Journal of Psychiatry, showed a greater improvement than in patients receiving standard therapy.
British experts said music may engage people in ways that words cannot.
Music therapists are used, including by the NHS, to help children who struggle to communicate. Playing instruments and singing with a trained music therapist is supposed to help children express themselves.
Initial improvement In this study, all patients with depression received the standard practice of counselling and appropriate medication. Thirty three of them were also given 20 sessions with a trained music therapist, which involved things such as drumming.
After three months, patients receiving music therapy showed a greater improvement in scores of anxiety and depression than the other set of patients.
However, there was no statistical improvement after six months.
Professor Christian Gold, from the University of Jyväskylä, said: "Our trial has shown that music therapy, when added to standard care helps people to improve their levels of depression and anxiety."
"Music therapy has specific qualities that allow people to express themselves and interact in a non-verbal way - even in situations when they cannot find the words to describe their inner experiences.
Dr Mike Crawford, who specialises in mental health services at Imperial College London, said in a journal editorial: "The results suggest that it can improve the mood and general functioning of people with depression.
"Music-making is social, pleasurable and meaningful. It has been argued that music making engages people in ways that words may simply not be able to."

APPRECIATION...


Professor Samuel Stephen Mushi
---
Professor Samuel Stephen Mushi
24th December, 1939 – 23rd July, 2011
The family of the Late Professor Samuel Stephen Mushi, would like  to thank  the Almighty  God for the life of our beloved father Professor Samuel Mushi, who passed  away on Saturday 23rd July 2011   at Muhimbili National Hospital in Dar-es-Salaam, and  laid to rest at his farm at Bunju B in Dar-es-Salaam on 27th July 2011.

May our sincere heartfelt gratitude go to the President of the United Republic of Tanzania, Vice President of the United Republic of Tanzania, Former President Benjamin William Mkapa, Former Prime Minister Frederick Sumaye, First Lady Mama Salma Kikwete, Staff of  Muhimbili National Hospital  and  Mikocheni Hospital, Pastors and Evangelists of Msasani  Lutheran church, Chancelor, Vice  Chancellor,  staff  and students of the department of Political Science and Public Administration and all the staff of the University of Dar-es-Salaam, Dar-es-Salaam Prime High School, Msasani, and Magomeni Choirs, Media houses, family and friends for their moral support, sympathy, love and encouragement as  we went through this time of grief.

We also thank everyone who fully participated and consoled us and rest assured GOD will grace your kindness and love.

“The Lord is my light and my salvation whom shall I fear? The Lord is the strength of my life; of whom shall I be afraid? “(PSALM 27:1)
Solely you will be missed by your wife Felister; your children Ukundi, Anande, Susan and Charles ;In laws; grandchildren; family, friends and all  others  you touched their lives at social and academic  world. Your humility, passion, love and humanity will be cherished and live for ever.

May Almighty God rest his soul in eternal peace.

AMEN

Tamko la Kamati Kuu ya CCM

 KATIBU WA NEC, ITIKADI NA UENEZI CCM, Bw Nape Nnauye
--
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imemaliza kikao chake cha siku moja usiku wa tarehe 31/07/2011 mjini Dodoma chini ya uenyekiti wa  Mwenyekiti wa CCM Taifa, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.

Pamoja na mambo mengine Kamati Kuu imeamua yafuatayo;

1.    Imefanya uteuzi wa makatibu  ishirini na saba (27) kujaza nafasi zilizokuwa wazi katika wilaya hizo. (majina na wilaya zao yameambatanishwa). Pamoja na uteuzi huo, Kamati Kuu imetengua uteuzi wa Makatibu wa Wilaya watatu (3) katika kuboresha ufanisi wa kazi katika wilaya hizo.(majina na wilaya zao yameambatanishwa).

2.    Kamati Kuu imepokea na kuridhia taarifa ya kujiuzulu kwa       aliyekuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kuwakilisha Mkoa wa Tabora, Ndugu Rostam Aziz. Aidha imempongeza kwa uamuzi huo uliozingatia maslahi mapana ya chama chake.

3.    Kamati Kuu imepokea pia taarifa ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Mbunge wa Igunga, Ndugu Rostam Aziz na kuagiza chama kupanga ratiba ya mchakato wa kumpata mgombea ubunge wa Jimbo la Igunga itakayozingatia ratiba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi juu ya uteuzi wa mgombea.

Aidha Kamati Kuu imeagiza shughuli zote za kampeni kutafanywa na CCM Mkoa, Wilaya na ngazi zote za chama wilayani Igunga. CCM Taifa watashiriki kuongeza nguvu. Chama kinatoa wito kwa wana CCM, wapenzi na wakereketwa wa chama chetu kushiriki kwa pamoja kuhakikisha jimbo linabaki kwa CCM.

4.    Kamati Kuu haijaridhishwa na kiwango cha bei ya mafuta ya taa nchini kwa kuwa ndio nishati inayotumiwa na wananchi wengi wenye kipato cha chini. Aidha Kamati Kuu haikuridhishwa na maelezo ya kupandishwa kwa bei ya mafuta hayo kwa kisingizo cha kuzuia uchakachuaji wa mafuta mengine.

Hivyo basi, Kamati Kuu imeiagiza Serikali kutafuta njia za kushusha bei ya mafuta ya taa na kuvitaka vyombo vya Serikali vinavyohusika na usimamiaji wa ubora wa mafuta, vihakikishe vinatimiza wajibu wake kuzuia kabisa mtindo wa uchakachuaji wa mafuta nchini na si kupandisha bei ya mafuta ya taa kama suluhisho.

5.    Kamati Kuu inasikitishwa na tatizo la umeme nchini kwani athari zake kwa uchumi wa Taifa na mtu mmoja mmoja ni kubwa. Hivyo basi imeitaka Serikali kutumia muda iliyopewa wa kurekebisha Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kuja na mpango wa dharura wa kunusuru hali hii na kisha kulimaliza kabisa tatizo la umeme nchini.

6.    Aidha Kamati Kuu imejadili masuala mengine kama; migogoro ya ardhi, tatizo la bei ya pamba, tatizo la uuzaji wa mahindi, migogoro migodini, masuala yanayohusu kero za Muungano na kuagiza Serikali kuyashughulikia kwani yanatatulika.

7.    Kamati Kuu imeipongeza Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa  kwa kazi nzuri ya kutekeleza maamuzi ya NEC na kuitaka iongeze kasi katika utekelezaji huo, ili kuhakikisha mageuzi yaliyokusudiwa yanatekelezwa kwa wakati. Aidha imejadili na kupitisha miundo mipya ya Idara ya Itikadi na Uenezi na Idara ya Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.

8.    Kuhusu suala la maadili ndani ya Chama, Chama kinaendelea kusimamia maadili, na kuwataka wale waliotakiwa kujipima na kuwajibika watumie muda huo, kujipima na kuwajibika kwa masilahi mapana ya chama.

Aidha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa inatarajiwa kukutana wakati wowote mwezi Septemba, ambapo pamoja na mambo mengine itatathimini utekelezaji wa maamuzi yake.


Imetolewa na:-

Nape M. Nnauye (MNEC)
KATIBU WA NEC, ITIKADI NA UENEZI
DODOMA
1/8/2011