Chama cha Mapinduzi leo kinazindua rasmi kampeni kwa ajili ya uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga mkoani Iringa. Uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika Ifunda kuanzia saa sita mchana. Mgeni rasmi katika uzinduzi huo ni Mwigulu Nchemba, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara. Mgombea katika jimbo hilo lililoachwa wazi na Dk. William Mgimwa kufuatia kifo chake, ni Godfrey Mgimwa.
No comments:
Post a Comment