KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Thursday, 27 February 2014

mj_36780.jpg
Nilikutana nae mitaa ya kati, Kariakoo leo mchana. Nikamwambia kaka yangu Juma Ikaangaa, mshindi wa medali ya fedha Commonwealth games, Brisbane Australia, 1982, mshindi wa nafasi ya kwanza New York Marathon, na mshindi wa mara tatu Boston Marathon, kwamba leo mimi niko fiti zaidi kuliko yeye, tukianza mbio mimi na yeye, tutoke Kariakoo hadi Magomeni,basi, nitakuwa wa kwanza kufika Magomeni wakati yeye akihangaika Jangwani...!
Tuache utani, Juma Ikangaa ni mmoja wa wanariadha walioliletea taifa hili sifa kubwa na kuitangaza Tanzania. Nakumbuka mwaka 1982 nilisoma makala Daily News iliyonisisimua sana kuhusu alichokifanya Juma Ikangaa, Brisbane, Australia, kwenye michuano ya Madola. Mwandishi mzungu aliandika, kuwa kule Brisbane, kwa jinsi Ikangaa alivyokimbia, walimwita Juma Ikanga-kangaroo! Leo nilimkumbusha Ikangaa hilo, alifurahi sana.
Na nikamwuliza Ikangaaa, hivi kweli, hii leo kama nchi, mbona hatuonekani kuwa tuna safari ya kwenda Glasgow, Scotland, kwenye Commonwealth games inayoanza July 3, 2014. Halafu tutakuja kulaumiana kuwa tumepeleka watalii watakaorudi mikono mitupu, bila hata medali za mbao!
Ikangaa naye hakuwa na majibu, bali kuonyesha masikitiko yake kwa jinsi miaka hii kusivyokuwa na umakini katika maandalizi, kulinganisha na wakati wake.

No comments:

Post a Comment