KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Thursday, 3 November 2011

DK Kimei: Serikali inatukwamisha

 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk Charles Kimei akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu hali ya kiuchumi ya benki hiyo. Kulia ni Katibu wa Benki hiyo John Bigambo. Picha na
Mwandishi Wetu
MGAWO wa umeme, kushuka thamani kwa shilingi ya Tanzania na ongezeko la mfumuko wa bei kulikofikia asilimia 17 na ongezeko la gharama za uendeshaji zimetajwa kuwa miongoni mwa changamoto zilizosababisha kupungua kwa uwezo wa wateja kulipa mikopo katika benki.

Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dk Charles Kimei alibainisha hayo jana katika mkutano na waandishi wa habari ambapo alieleza hali ya kibiashara ya benki hiyo katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Oktoba 31, ambapo alisema pamoja na changamoto hizo hali ya benki hiyo ni nzuri.

Dk Kimei alitaja changamoto nyingine kubwa kuwa ni Serikali kuchelewesha malipo kwa wakandarasi akiitaja Tanroads aliyosema inadaiwa zaidi ya bilioni 400 na kwamba hali hiyo inamaanisha kuwa sehemu kubwa ya mzigo huo wa madeni zinadaiwa mabenki.

"Kuongezeka kwa mfumuko wa bei kutoka asilimia 6.4 mwanzo wa mwaka wa 2011 hadi asilimia 17.4 mwishoni mwa mwezi Septemba 2011, kushuka kwa thamani ya shillingi ya kitanzania  kwa karibu ya asilimia 20 dhidi ya fedha za kigeni hasa hasa dola ya Marekani na mgawo wa umeme unaosababisha kuongezeka kwa gharama za uendeshaji, na kupungua kwa uwezo wa wateja wetu wakopaji kuzalisha na kulipa mikopo yao,"alisema Dk Kimei.  

Hata hivyo mkurugenzi mtendaji huyo wa CRDB alisema, hadi kufikia mwisho wa mwezi Septemba mwaka huu benki hiyo ilikuwa na amana za wateja zilizofikia Sh2.3 trilioni, wakati  katika mwezi Juni katika robo ya pili ya mwaka 2011ilikuwa na amana za zipatazo Sh2.1 trilioni, hivyo kuwa na ongezeko la Sh200 bilioni.

Kuhusu mikopo, Dk Kimei alisema hadi kufikia mwisho wa robo ya tatu ya mwaka 2011, CRDB imetoa mikopo inayofikia Sh1.3 trilioni ikiwa ni ongezeko la Sh80 bilioni na kwamba katika kipindi hicho benki hiyo imepata faida ya Sh63 bilioni 63 kabla ya kodi.

No comments:

Post a Comment