MGAWO wa umeme, kushuka thamani kwa shilingi ya Tanzania na ongezeko la mfumuko wa bei kulikofikia asilimia 17 na ongezeko la gharama za uendeshaji zimetajwa kuwa miongoni mwa changamoto zilizosababisha kupungua kwa uwezo wa wateja kulipa mikopo katika benki. Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dk Charles Kimei alibainisha hayo jana katika mkutano na waandishi wa habari ambapo alieleza hali ya kibiashara ya benki hiyo katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Oktoba 31, ambapo alisema pamoja na changamoto hizo hali ya benki hiyo ni nzuri. Dk Kimei alitaja changamoto nyingine kubwa kuwa ni Serikali kuchelewesha malipo kwa wakandarasi akiitaja Tanroads aliyosema inadaiwa zaidi ya bilioni 400 na kwamba hali hiyo inamaanisha kuwa sehemu kubwa ya mzigo huo wa madeni zinadaiwa mabenki. "Kuongezeka kwa mfumuko wa bei kutoka asilimia 6.4 mwanzo wa mwaka wa 2011 hadi asilimia 17.4 mwishoni mwa mwezi Septemba 2011, kushuka kwa thamani ya shillingi ya kitanzania kwa karibu ya asilimia 20 dhidi ya fedha za kigeni hasa hasa dola ya Marekani na mgawo wa umeme unaosababisha kuongezeka kwa gharama za uendeshaji, na kupungua kwa uwezo wa wateja wetu wakopaji kuzalisha na kulipa mikopo yao,"alisema Dk Kimei. Hata hivyo mkurugenzi mtendaji huyo wa CRDB alisema, hadi kufikia mwisho wa mwezi Septemba mwaka huu benki hiyo ilikuwa na amana za wateja zilizofikia Sh2.3 trilioni, wakati katika mwezi Juni katika robo ya pili ya mwaka 2011ilikuwa na amana za zipatazo Sh2.1 trilioni, hivyo kuwa na ongezeko la Sh200 bilioni. Kuhusu mikopo, Dk Kimei alisema hadi kufikia mwisho wa robo ya tatu ya mwaka 2011, CRDB imetoa mikopo inayofikia Sh1.3 trilioni ikiwa ni ongezeko la Sh80 bilioni na kwamba katika kipindi hicho benki hiyo imepata faida ya Sh63 bilioni 63 kabla ya kodi. | Mwandishi Wetu
KARIBUNI
Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.
Thursday, 3 November 2011
DK Kimei: Serikali inatukwamisha
Serikali yakataa ushoga
|
Waziri Membe asema kama ni misaada yao basi Raymond Kaminyoge TANZANIA imesema ipo tayari kukosa misaada yote kutoka Serikali ya Uingereza na kamwe haiwezi kuruhusu sheria inayotambua mashoga na kuhalalisha ndoa za jinsia moja.Msimamo huo mzito wa serikali umekuja siku chache baada ya Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron, kutamka kwamba nchi yake ina mpango wa kusitisha misaada yake kwa nchi ambazo sheria na katiba zao, hazitambui mashoga na ndoa za jinsia moja. Cameron alikaririwa akithibitisha kuwa tayari amewajulisha juu ya suala hilo Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola waliokuwa wakihudhuria mkutano wa Jumuiya hiyo uliomalizika siku nne zilizopita, mjini Perth , Austaralia ambao pia ulihudhuriwa na Rais Jakaya Kikwete. Waziri Mkuu huyo kutoka chama cha Conservative ambacho kilishinda uchaguzi Mei mwaka jana, alisema suala hilo la mashoga na ndoa za jinsi moja ni moja ya mambo yanayoongoza sera ya serikali yake kuhusu misaada kwa mataifa mbalimbali na kwamba tayari imeanza kutekelezwa katika maeneo kadhaa duniani. Kauli ya Cameron imechukuliwa kama kielelezo cha ukoloni mamboleo ambao Uingereza inajaribu kuupandisha daraja kwa mataifa yanayoendelea kwa kigezo cha misaada Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe, alisema pamoja na umasikini wake, Tanzania kamwe haitaruhusu upuuzi huo kwa kigezo cha misaada. “ Tanzania ni nchi maskini lakini hatutakubali kuruhusu upuuzi huo eti kwa sababu ya misaada yake na fedha zao, lakini ushoga si utamaduni wetu, hata sheria zetu zinakataa,” alisema Membe. Alifafanua kuwa katika kuonesha msimamo wa kutokukubaliana na masharti hayo, Tanzania imeshikilia msimamo thabiti kupinga upuuzi huo ambapo Januari mwaka huu, ilimkataa balozi shoga ambaye aliteuliwa na nchi yake kuja kuiwakilisha hapa nchini. Hata hivyo Waziri Membe hakutaja jina la balozi huyo wala nchi anayotoka. “Niwape siri moja ambayo tuliificha lakini leo ngoja niwaambie, mwanzoni mwa mwaka jana nililetewa barua kunijulisha ujio wa balozi mmoja anayekuja kuiwakilisha nchi yake, mwanamume mwenye ndoa ya jinsia moja. Nilikwenda kumweleza Rais Jakaya Kikwete kuhusu wasifu wa balozi huyo mtarajiwa naye akajibu kwa maneno matatu, yarabi toba! Mkatae!” Waziri Membe alifafanua kuwa serikali ilimkataa balozi huyo kwa kuwa ni kinyume cha utamaduni wetu na sheria za nchi kuwa na watu wenye tabia hizo. Alisema alimjulisha waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo kwamba balozi huyo haruhusiwi kuja kufanya kazi nchini kwa kuwa ni kinyume na utamaduni wetu. “ Waliendelea kuniomba kwamba balozi huyo akija hatatoka kwenye makazi yake akiwa na mwenza wake hivyo watu hawatamuona lakini tulimkataa kabisa, wakatuelewa,” alisema Membe. Alieleza kuwa tamko hilo la Waziri Mkuu Cameron linaweza kusababisha hatari ya kuvunjika kwa uhusiano miongoni mwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola na koloni mama Uingereza na waziri huyo atabeba lawama hizo Akisisitiza msimamo huo wa serikali, Membe, alisema Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 kifungu cha tisa, kinatambua ndoa ya jinsia mbili tofauti, yaani mume na mke. “ Sheria hizi tunazozitumia hivi sasa tumezirithi kutoka Uingereza ambako leo wanatukuza ndoa za jinsia moja na ushoga,” alisema Membe. Suala la kile kinachoitwa haki za binadamu kuhusu ushoga ilikuwa moja ya ajenda ambazo viongozi kadhaa walishindwa kuafikiana katika mkutano Perth . Hoja ya kukomesha vizuizi dhidi ya ushoga na ndoa za jinsi moja lilikuwa moja ya mapendekezo yaliyokuwamo katika ripoti ya ndani kuhusu matarajio ya baadaye ya Jumuiya hiyo ya Madola. Itakumbukwa kwamba, Malawi tayari imeathirika na mpango huo wa Uingereza kwa sehemu ya misaada yake kusitishwa kutokana na msimamo wa nchi hiyo kuhusu kile Uingereza na nchi za Magharibi zinazokiita haki za mashoga. Ikumbukwe pia kuwa, mjadala mzito ulioibuka katika Bunge la Uganda mwaka 2009 kuhusu ndoa za jinsi moja ilikuwa sehemu ya utekelezaji wa sera hiyo ya Uingereza na washirika wake. Ajenda zingine Mkutano wa Perth Waziri Membe alisema viongozi wa Jumuiya ya Madola walikubaliana suala la mabadiliko ya tabia nchi kuwa ajenda kuu katika nchi hizo. Alisema ajenda hiyo sasa inakuwa muhimu kutokana na nchi nyingi wanachama wa jumuiya hiyo kuwa katika tishio kubwa la uharibifu wa mazingira. Aidha, Membe alisema nchi hizo zimekubaliana kuandaa kanuni na mwongozo ambao utatakiwa kufuatwa na nchi za jumuiya hiyo. “ Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Jumuiya ya Madola tutakutana Aprili mwakani kuandaa miongozo na kanuni hizo,” alisema Membe. mwisho |
Waziri Mkuu Mizengo Pinda Akutana na Balozi Finland Nchini Tanzania
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda kisalimiana na Balozi Finland nchini, Mhe Sinikka Antila kabla ya mazungumzo yao, ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Novemba 3,2011.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,Maalim Seif Akutana na Mwakilishi wa UNDP
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,Maalim Seif Sharif Hamad akibadilishana mawazo na mwakilishi wa UNDP bibi Ana Barradas wakati ujumbe wa Shirika hilo ulipofika Ofisini kwake Migombani kujadiliana juu ya Tathmini ya uchaguzi mkuu uliopita.
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad akibadilishana mawazo na ujumbe wa UNDP uliofika ofisini kwake Migombani kutathmini juu ya hali ya uchaguzi uliopita.
--
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amesifu ustaarabu na hali ya kuvumiliana iliyokuwepo wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita.
Amesema hali hiyo ilipelekea uchaguzi uliopita kufanyika kwa utulivu mkubwa na kuiletea sifa kubwa Zanzibar ambayo ilikuwa ikikumbwa na vurugu kila ifikapo kipindi cha uchaguzi.
Maalim Seif ameeleza hayo leo Ofisini kwake migombani mjini Zanzibar alipokuwa na mazungumzo na ujumbe wa shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP bibi ANA BARRADAS kuhusiana na tathmini ya shirika hilo kwa uchaguzi uliopita.
Amebainisha kuwa licha ya kuwepo mafanikio katika kipindi chote cha kampeni na uchaguzi kwa jumla, uchaguzi huo ulikuwa na kasoro ndogo ndogo ambazo zinapaswa kurekebishwa ili kujenga mazingira bora zaidi katika uchaguzi ujao.
Ametaja baadhi ya kasoro hizo kuwa ni pamoja na baadhi ya wananchi kutopata fursa ya kupiga kura kutokana na kukosa vitambulisho vya uzanzibari ukaazi pamoja na kutokuwepo na uwazi katika hatua za mwisho za kujuisha matokeo.
Amesema wakati umefika kwa taasisi zinazohusika kurekebisha kasoro hizo ili chaguzi zijazo zifanyike katika misingi ya uwazi na haki na kumfanya kila mmoja kuridhishwa na mchakato wa uchaguzi.
Akizungumzia hali ya siasa baada ya uchaguzi Maalim Seif amesema imepata mafanikio makubwa kwani vyama vya CCM na CUF vimekuwa vikifanya kazi kwa pamoja na kuweka kando tofauti zao katika kuangalia mustakbali wan chi.
“Mfano mzuri ni kuundwa kwa Jumuiya ya Maridhiano Zanzibar (ZAMA). Jumuiya hii inawahusisha vijana wa CCM na CUF na inafanya kazi vizuri sana kwa mashirikiano”, amedokeza maalim Seif.
Makamu wa kwanza wa Rais amelishukuru shirika hilo kwa kuunga mkono uchaguzi uliopita na kuliomba kutoa misaada yake mapema ili kurahisisha mchakato wa uchaguzi kuanzia hatua za awali na kuipelekea Zanzibar kuendesha chaguzi kwa misingi ya demokrasia ya kweli.
Amesema ipo haja kwa shirika hilo kusaidia elimu ya uraia hasa kwa wananchi wa vijijini, kwani wananchi wengi wa maeneo hayo wamekuwa wakikosa uelewa juu ya mchakato wa uchaguzi na kupelekea kuharibika kwa kura nyingi na kushindwa kufanya maamuzi sahihi katika uchaguzi.
Nae kiongozi wa ujumbe huo bibi ANA BARRADAS amesema ameridhishwa na hali ya siasa za Zanzibar baada ya uchaguzi, hali ambayo inafaa kuendelezwa kwa maslahi ya wananchi na taifa kwa jumla.
Aidha ameahidi kuwa shirika litaendelea kushirikiana na Zanzibar katika kufanikisha chaguzi za kidemokrasia nchini.
IMETOLEWA NA:
Hassan Hamad
Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
SWAHILI FASHION WEEK OFFICIALLY LAUNCHED IN KENYA
Mustafa Hassanali briefing the Media, on his left is USAID Compete Representative Finn Holm-Olsen and on the right Redd's Kenya Marketing Manager Pinkie Nyandoro
Redd's Kenya Marketing Manager Pinkie Nyandoro Addressing the Media, on her right is USAID Compete Representative J C Mazingue
Cross section of kenyan Media who attended the Swahili Fashion Week media Briefing on Nov 2 hosted by Redd's original
---
Swahili Fashion Week, East and Central Africa largest fashion event, now in its Fourth year, will be held at The National Museum on the 10th, 11th and 12th November 2011 in Dar Es Salaam, Tanzania.
Swahili Fashion Week 2011 will collectively bring together 50 fashion and accessories designers from Swahili speaking countries and beyond to showcase their creativity and forecast future fashion trends for the region.
“Over the years since its inception in 2008, we have grown tremendously, and now we look towards regional integration of the East Africa Member states using the Fashion industry , Thus Launching Officially Swahili Fashion week – Kenya Chapter this year especially when we celebrating 50 years of Tanzanian Independence” stated the founder of the Fashion week Mustafa Hassanali. When he addressed the Kenyan Media on 2 November 2011 at a reception hosted by REDD’S in Nairobi
Four Kenyan Designers have been invited to showcase at this event, namely Patricia Lulu Mbela of Poisa, Rachel Mutindi of KI2 Collection, Vera vee Ochia from Malindi and Sonu Sharma of just Like that.
“Being the drink of choice for the discerning woman, REDD’S Original, wishes the Kenyan designers showcasing at Swahili fashion week the very best and we hope they shall showcase Kenyan creativity to its best” stated Redd’s Marketing manager Pinkie Nyandoro
In addition to the Fashion Show presentations, Swahili Fashion Week Shopping Festival which was incorporated in year 2010 will once again be the main feature and up to date more than 40 exhibitors participating thus making it the largest shopping festival in the country.
“Opening Swahili Fashion Week to a new audience, and keeping to the tradition of being first, this year we shall unveil the first ever Fashion Awards in East and Central Africa celebrating achievements made by the fashion industry stakeholders not only in the Tanzania but also in the region ”, added Hassanali
In the Best East African Designer category, nominees from Kenya are Wambui Njogu of MOO COW, Anne Mcreath of KIKO ROMEO, Patricia Mbela of POISA and John Kaveke.
“Being Truly East African, Precision Air, Tanzania Largest and Fastest Growing Private airline truly embodies the value of regional integration, hence being the Official Airline of the Region Largest Fashion event, we look forward to promoting the Fashion Industry within East Africa.” Stated Precision Air Country manager Sarah Wachira.
USAID Compete Have played a pivotal role in the Swahili Fashion Week by Empowering the Knowledge of the Various Industry stakeholders as to how to integrate marketing with Fashion, building World Class East African Brands.
“With our Ambitious plan to promote the Business of Fashion in the region, I would like to thank all our Partners, some of whom have supported us from the past previous Years to-date in Our initiative to develop , nurture and foster growth of the regions fashion and textile industry “ Concluded Mustafa
Swahili fashion week 2011 has been sponsored by USAID – Compete, Origin Africa home of Swahili Fashion Week - Southern Sun, EATV, East Africa Radio, Precision Air, BASATA (Baraza La Sanaa Tanzania), Amarula, Ultimate Security, REDD’S original, Image Masters, Global Outdoor Ltd, Vayle Springs Ltd, Eventlites, Nipashe, Perfect Machinery Ltd, Michuzi blog, PKF Tanzania, photo point and 361 Degrees.
Mkurugenzi Mtendaji Mpya Wa Vodacom Tanzania Amtembelea Waziri Mkuu Mizengo Pinda
Written by haki | // 0 comments
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji Mpya wa Kampuni ya simu za Mikononi ya VODACOM Bw.Rene Meza kabla ya mazungumzo yao,ofisini kwake jijini Dar es salaam Novemba 3,2011 Katikati ni Ofisa Mkuu wa VODACOM TANZANIA, Mwamvita Makamba.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji Mpya wa Kampuni ya simu za Mikononi ya VODACOM Bw. Rene Meza, ofisini kwake jijini Dar es salaam Novemba 3, 2011. Katikati ni Ofisa Mkuu wa VODACOM TANZANIA, Mwamvita Makamba.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji Mpya wa Kampuni ya simu za Mikononi ya VODACOM Bw. Rene Meza, ofisini kwake jijini Dar es salaam Novemba 3, 2011. Katikati ni Ofisa Mkuu wa VODACOM TANZANIA, Mwamvita Makamba.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Sheria wa kampuni ya Vodacom Bw. Walarick Nittu wakati Mkurugenzi Mendaji mpya wa Vodacom Tanzania Bw. Rene Meza (wa pili kulia) alipomtembelea Waziri Mkuu ofisini kwake jijini Dar es salaam leo kujitambulisha. Wa pili kushoto ni Ofisa Masoko Mkuu na Mahusiano wa Vodacom Bi. Mwamvita Makamba.
Subscribe to:
Posts (Atom)