KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Monday, 18 February 2013

MEZA YA MAGAZETI LEO JUMANNE

    g 002 e1b2e

g 003 57a8b
g 004 a6684
g 005 e9a20
g 006 a9e5b

Rais Kikwete ana Hasira, Wanaosema Mpole Hawamjui – Mama Salma Kikwete.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
NA BASHIR NKOROMO, LINDI
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ametoboa siri kwamba mumewe, Rais Jakaya Kikwete pamoja sura yake kujawa haiba ya ucheshi wa mara kwa mara lakini kwa tabia ana hasira.
Amesema, Rais Kikwete hukasirika sana anapoona au kusikia mtu au mtendaji katika Chama au serikali anafanya mambo ya hovyo au ya kizembe hasa katika masuala ya kazi.
Mama Salma Kikwete ametoboa siri hiyo, jana Februari 18, 2013, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Kikwetu Kata ya Mbanja akiwa katika ziara ya kukagua, kuimarisha uhai wa chama, kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama na kuwashukuru wana-CCM wa Lindi mjini kwa kumchagua kuwa mjumbe wao wa NEC.
“Siyo kweli kwamba Rais Jakaya Kikwete siyo mkali, japokuwa ana sura yenye haiba ya ucheshi wa mara kwa mara kwa kila mtu, lakini ni ana hasira tena  sana pale mtendaji au mtu yeyote anapombaini kwamba anafanya mambo ya hovyo ay ya kizembe katika kazi za Chama au serikali yake”, alisema Mama Salma Kikwete.
Mama Kikwete akitoa ufafanuzi, baada ya mshereheshaji mmoja kwenye mkutano huo Mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Lindi mjini Muhsin Ismail, kusema kwamba Rais Jakaya Kikwete ni mpole wa kupindukia na kuuliza umati wa wananchi waliokuwa kwenye mkutano huo kwamba je ni nani amewahi kumuona amenuna.
“Natoa ofa kama hapa kuna mtu aliyewahi kumuona mpendwa wetu, Rais Kikwete amenuna anyooshe mkono. Akitokea ntampa sh. elfu moja hapa hapa… Kwa mara ya kwanza, ya pili unaona hakuna”, alisema Muhsini.
Wakati akiendelea kusema hivyo, mtu mmoja kwenye mkutano huo alinyoosha mkono, lakini Muhsin akakataa kumpa zawadi yake kama alivyokuwa ameahidi. “Aaa wewe sikupi zawadi”, alisema Muhsini lakini papo hapo akakatishwa na Mama Salma Kikwete.
“Hata kama humpi hiyo zawadi, sawa. lakini Siyo kweli kwamba Rais Jakaya Kikwete hakasiriki na siyo mkali. Japokuwa ana sura yenye haiba ya ucheshi wa mara kwa mara kwa kila mtu, lakini ana hasira, tena  sana pale mtendaji au mtu yeyote anapombaini kwamba anafanya mambo ya hovyo na ya kizembe…” alisema Mama Kikwete.

Breastfeeding Could Save 95 Babies Every Hour.

The lives of 95 babies could be saved every hour if mothers started breastfeeding their newborns in the hour after their birth.
Receiving a mother’s first milk within an hour will kick start the child’s immune system, making a newborn three times more likely to survive.
According to a report by Save the Children, if the mother continues feeding for the next six months, then a child growing up in the developing world is up to 15 times less likely to die from killer diseases such as pneumonia and diarrhea..
 According to the charity, there has been enormous progress in reducing child mortality, but more could be done if mothers were encouraged to breastfeed.
According to the report, called Superfood For Babies, Breastfeeding rates are declining across East Asia and in some of Africa’s most populous countries such as Ethiopia and Nigeria. 

Sikika yampongeza Waziri Mwinyi kwa Kuwajibika.

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi.
Sikika inapenda kumpongeza Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi kwa kuweka bayana na kukiri kwamba kuna uhaba mkubwa wa dawa muhimu za kutibu malaria, maarufu kama dawa mseto (Alu) katika vituo vingi vya huduma za afya vya umma nchini.
Akizungumza na vyombo vya habari hivi karibuni, waziri Mwinyi alikiri kuwepo kwa uhaba wa dawa hizo za kutibu malaria kama zilivyoripotiwa na mtandao wa Wizara hiyo kupitia mfumo wa kielektroniki ujulikanao kama ‘SMS for Life.’ Dk. Mwinyi alinukuliwa  akiwataka watanzania kutokuwa na wasiwasi kwani suala hilo lilikuwa linashughulikiwa na kwamba usambazaji wa Alu ulishaanza.
Tunampongeza kwa dhati waziri Mwinyi kwa  kukiri uwepo wa tatizo hili na kuchukua hatua. Sikika tunaamini kwamba hatua hiyo  ni muhimu katika kukuza uwajibikaji na uwazi. Wiki mbili zilizopita, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Regina Kikuli na Msemaji wa wizara hiyo, Nsachris Mwamwaja walikanusha taarifa iliyotolewa  na Sikika kwamba kuna uhaba wa Alu   kwa takribani asilimia 26, katika vituo vya huduma za afya nchini.  Taarifa hizo zilipakana kutoka kwenye  mfumo huo huo wa Wizara (SMS for life).
Taarifa ya Kikuli pia ilikaririwa na vyombo vya habari ikiueleza  umma kwamba kuna dawa nyingine za malaria ambazo haziripotiwi kupitia SMS for life, jambo ambalo si kweli.
Sikika inaiomba Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuharakisha usambazaji wa dawa hizi na ilichukulie suala hili kama dharura kwani kuna baadhi ya vituo vya huduma vina uhaba mkubwa wa Alu kwa takribani siku 300 sasa. Pia tunaishauri Wizara kubadili mfumo wa uagizaji wa dawa kwa zahanati na vituo vya afya  ambao huvilazimu vituo kuagiza dawa kila baada ya miezi mitatu (robo mwaka), wakati usambazaji wake unachukua muda wa miezi miwili hadi mitatu. Ni vyema vituo viwe vinaagiza dawa kila mwezi ili kupunguza tatizo la uhaba wa dawa muhimu unaojitokeza mara kwa mara.
Ikumbukwe kwamba msimu wa mvua unakaribia kuanza katika maeneo mengi hapa nchini na hivyo kuwepo kwa uwezekano wa kuongezeka kwa maambukizi ya malaria. Ugonjwa wa malaria unaongoza kwa kusababisha vifo vingi nchini.  Hivyo basi,  uwepo wa dawa za ALu za kutosha katika vituo vya huduma utasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza vifo hivyo.
Ni jambo la kushangaza kuona kuwa ALu zinakosekana katika vituo vingi hapa nchili wakati kuna fedha za kutosha kutoka kwa wafadhili kwa ajili ya ununuzi wa dawa hizo. Kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita, Tanzania ilipokea kiasi cha dola za Marekani 331,112,207 kutoka Global Fund pekee, ambapo kiasi cha dola za Marekani 294,975,327 tayari zimeshatumika. Ukiachilia mbali Global fund, malaria pia imekuwa ikifadhiliwa na Mfuko wa Ufadhili wa Rais wa Marekani (PMI – USAID), Benki ya Dunia (World Bank) pamoja na wahisani wengine.
Yapo makampuni makubwa manne ambayo yameteuliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa ajili ya kuleta dawa hizo hapa nchi. Makampuni haya yanatambulika kimataifa kwa kuwa na uwezo mkubwa wa kuzalisha na kusambaza dawa hizo kwa vipindi maalum. Tatizo tunaloliona hapa ni Wizara yetu kushindwa kufanya makadirio na kuagiza dawa hizo kwa wakati.
Ni wakati sasa kwa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria (NMCP), Bohari ya Dawa ya Taifa (MSD), Kitengo cha Dawa cha Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii (PSS) na Waganga Wakuu wa Wilaya (DMOs) kuchukua hatua madhubuti za kutatua tatizo la uhaba wa Alu. Suluhu ya tatizo hili ni kwa wote wanaohusika kuwajibika kwa dhati ili kuokoa maisha ya watanzania.
Vilevile, tunaishauri serikali kupanua wigo wa matumizi ya mfumo wa ‘SMS for Life’ ili kuongeza dawa zingine muhimu na vifaa tiba. Mfumo huu unasaidia sana kutoa taarifa zenye ukweli na uhalisia na kuhusu uhaba wa dawa ili wizara  ijipange kukabiliana na tatizo hilo kwa kusambaza dawa zinazohitajika kwa wakati. Mfumo huu pia utasaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha uwazi na uwajibikaji katika usambazaji wa dawa,  hatimaye kuboresha utoaji wa huduma za afya nchini.
Kwa namna ya pekee, Sikika inavipongeza vyombo vya habari kwa juhudi zao za dhati katika kuuhabarisha umma juu ya tatizo la uhaba wa Alu. Vyombo hivyo vilitanguliza zaidi maslahi ya umma bila kujali matamko ya wazi ya baadhi ya viongozi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ya kuupindisha ukweli. Kwa mara nyingine tena, vyombo vya habari vimeweza kuonesha uzalendo kwa kuweka maslahi ya taifa mbele. 
Mr. Irenei Kiria, Mkurugenzi wa Sikika, S.L.P 12183 Dar es Salaam,
Simu: +255 222 666355/57, Nukushi: 2668015, Barua pepe: info@sikika.or.tz,
Twitter: @sikika1, Facebook: Sikika Tanzania, Tovuti: www.sikika.or.tz

WanaCCM Gongo la Mboto wampongeza Jerry Silaa kwa kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.

Baadhi ya  kinamama wa Gongo la Mboto ambao ni wananchama wa CCM wakiwasili kwenye Uwanja  uliopo karibu na reli Gongo la Mboto katika mkutano wa hadhara wa kumpongeza Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto Jerry Silaa baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa. (Picha na Zainul Mzige wa Mo Blog).
Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmshauri Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Mstahiki Meya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akisalimiana na waendesha Boda boda wa Gongo la Mboto waliofika kumlaki akitokea mjini Dodoma.
Msafara wa waendesha Boda boda ukimsindikiza Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Jerry Silaa kwenye viwanja vya Gongo la Mboto alipoandaliwa sherehe ya kumpongeza iliyoenda sambamba na mkutano wa hadhara.
Watoto waliokuwa pembezoni mwa barabara wakimpungua kwa furaha Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Jerry Silaa alipokuwa akipita na msafara wake.
Pichani Juu na Chini ni baadhi ya viongozi wa CCM wakimlaki Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Jerry Silaa katika Ofisi za CCM kata ya Gongo la Mboto alipopita kutia baraka ofisi hizo akielekea kwenye mkutano wa hadhara ulioandaliwa kwa ajili ya kumpongeza.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala na Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmshauri Kuu ya CCM Taifa Jerry Silaa akitia saini kitabu cha wageni cha Ofisi za CCM kata ya Gongo la Mboto.
Waendesha boda boda wa Gongo la Mboto wakitia mbwembwe katika mkutano wa hadhara ulioenda sambamba na sherehe za kumpongeza Jerry Silaa aliyeteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Mh. Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Msafara wa Jerry Silaa ukiwasili uwanjani hapo kwenye mkutano wa hadhara na wananchi wa Gongo la Mboto.
Mjumbe wa kamati kuu na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Jerry Silaa akipunga mkono kwa wananchi, WanaCCM waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara ulioenda sambamba na sherehe za kumpongeza kuchaguliwa nafasi nyeti ya Chama cha Mapinduzi.
Mjumbe wa Kamati kuu na Halmashauri kuu ya CCM taifa Jerry Silaa akivishwa skafu ya chama mara baada ya kuwasili kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Gongo la Mboto.
Jerry Silaa akivishwa lubega ya kimasai baada ya kuwasili kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jana Gongo la Mboto jijini Dar.
Pichani juu na chini ni Baadhi WanaCCM wa kata ya Gongo la Mboto wakimpongeza Jerry Silaa baada ya kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati kuu na Halmashauri kuu ya CCM Taifa wakati wa mkutano wa hadhara ulioenda sambamba na sherehe za kumpongeza katika viwanja vya Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya umati wa wakazi wa Gongo la Mboto wakubwa kwa wadogo waliohudhuria mkutano wa hadhara ulioenda sambamba na sherehe za kumpongeza Jerry Silaa.
Wanenguaji wa Mashujaa Band wakicheza staili ya Boda boda na Wana CCM wa Gongo la Mboto wakati wa mkutano wa hadhara.
“UTU UZIMA DAWA KWA RAHA ZETU”…Rappa wa Bendi ya Mashujaa akicheza sambamba na kinamama wa Kata ya Gongo la Mboto wakati wa sherehe za kumpongeza Jerry Silaa zilizoenda sambamba na mkutano wa hadhara.
Jukwaa kuu la viongozi mbalimbali wa chama cha Mapinduzi (CCM) walioshiriki katika mkutano wa hadhara uliofanyika mwishoni mwa wiki Gongo la Mboto jijini Dar.
Katibu Mwenezi wa CCM Mtwara Bw. Haroun Maarifa akitoa salamu kwa wana CCM wa Gongo la Mboto wakati wa mkutano wa hadhara ulioenda sambamba na sherehe za kumpongeza Jerry Silaa.
Wana CCM wa Gongo la Mboto wakitia manjonjo kwenye mkutano huo.
Mbunge wa Ukonga Mh. Eugene Mwaiposi akizungumza na wananchi wa Gongo la Mboto wakati wa mkutano wa hadhara ulioenda sambamba na sherehe za kumpongeza Jerry Silaa ambapo amezungumzia mambo mbalimbali ya maendeleo ya Wakazi wa jimbo lake yanayopangwa kufanywa na Serikali kwa manufaa ya wakazi wa maeneo hayo.
Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Abillahi Mlewa akizungumza machache na wananchi wa kata ya Gongo la Mboto kabla ya kumkaribisha Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa kuhutubia wananchi katika mkutano huo.
 Mjumbe wa kamati kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa Jerry Silaa akisindikizwa Jukwaani kwa staili ya aina yake ya kufagiliwa njia na WanaCCM waliokuwa wakibiringika mpaka kwenye ngazi za jukwaa. Anayemsindikiza ni Diwani wa Kata ya Tabata Hajati Mtumwa Mohamedi.
“Karibuni kwenye Chama chenye mshikamano na Sera za Ukweli” ndiyo maneno ya Mjumbe wa kamati kuu na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Jerry Silaa wakati akigawa kadi  kwa Wanachama wapya wa Gongo la Mboto walipoamua kujiunga baada ya kukolewa na sera za CCM wakati wa mkutano huo.
Zoezi la ugawaji kadi kwa wanachama wapya likiendelea. Kulia ni Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Abillahi Mlewa.
Pichani juu na chini ni Wanachama wapya wa CCM wakila kiapo mbele ya Mjumbe wa kamati kuu na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Jerry Silaa na viongozi mbalimbali wa Chama wakati wa mkutano wa hadhara ulioenda sambamba na sherehe za kumpongeza Jerry Silaa.
Mstahiki Meya wa manispaa ya Ilala ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto Mh. Jerry Silaa akizungumza na wananchi wa Kata yake ya Gongo la Mboto ambapo amewasihi viongozi wa CCM ngazi za Chini kuhakikisha wanafuatilia na kutafutia ufumbuzi  kero zinazo wakabili watu wanaowazunguka.
Mstahiki Meya ametumia fursa hiyo kuwashukuru wananchi na wana CCM kwa ujumla kufuatia kuteuliwa na Mh.rais kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na kusema ofisi za chama zinatakiwa kuwa wazi kuanzia ngazi ya kata mpaka mkoa ili wananchi waweze kufika kutoa kero zao.
Aidha amewataka viongozi wenzake kufanyakazi kwa ushirikiano na uadilifu, na kuwa wale viongozi wachache wasio waadilifu watashughulikiwa kikamilifu ili kuleta ufanisi ndani ya chama.
Baadhi ya wananchi wa Gongo la Mboto wakichukua taswira ya Diwani wao Jerry Silaa wakati wa mkutano wa hadhara.
Mmoja wachekeshaji katika mikutano ya CCM wanaofahamika kama Aki na Ukwa akimwombea Dua Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa mara baada ya kuzungumza na wana CCM wa Gongo la Mboto.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Jerry Silaa akisalimiana na wananchi wa Gongo la Mboto mara baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara.
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Jerry Silaa akisalimiana na mmoja wa watoto waliohudhuria kwenye mkutano wa hadhara.
“Asante kwa kuonyesha upendo…Mume wa mtu mie” ndivyo anavyoonekana kusema Mh. Jerry Silaa akimwambia mwana CCM mkereketwa aliyekwenda kumfuta jasho kwa kutumia Khanga yake.